UKIWATAJA wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu wenye umri mkubwa na majina Bongo, hutakosa kumtaja nguli wa filamu, Ahmed Olotu...
UKIWATAJA wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu wenye umri mkubwa na majina Bongo, hutakosa kumtaja nguli wa filamu, Ahmed Olotu maarufu kama ‘Mzee Chilo.’
Nguli wa filamu, Ahmed Olotu maarufu kama ‘Mzee Chilo.’
Mkongwe huyu mwenye miaka 65 aliyejikita kwenye tasnia ya filamu
tangu miaka 10 iliyopita na kujipatia umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya
ya Jumba la Dhahabu iliyokuwa ikirushwa na kituo cha TBC 1, enzi hizo
TVT, amefungukia mengi kuhusiana na tasnia ya uigizaji:
Una miaka mingapi kwenye tasnia ya filamu?
“Aah! Kwenye tasnia ya filamu, kuanzia tamthiliya hadi muvi nina miaka 10. Yaani hapo kuanzia enzi zilee za Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu mpaka sasa.”
Kabla ya kuanza kujihusisha na sanaa hii ya maigizo ulikuwa unafanya shughuli gani?
“Nilikuwa na shughuli mbalimbali za kiserikali na binafsi, nilifanya kazi ubalozini, halafu nikawa mwalimu na baadaye mfanyabiashara.”
Je, ni mafanikio gani uliyoyapata tangu ujiingize kwenye tasnia ya filamu?
“Kwanza sikutegemea kama ningefikia hapa, kwa ujumla nimejuana na watu wengi kiasi kwamba hata nikifika sehemu bila kuonesha kitambulisho nimekuwa nikiruhusiwa kuingia kwa kuwa uso wangu tu umekuwa ni dhamana, lakini pia hata sauti yangu tu imekuwa utambulisho tosha hata nikipiga simu watu wamekuwa wakiitambua sauti yangu. Hayo ni mafanikio makubwa sana kwangu. Lakini kwa ujumla sanaa hailipi sana.”
Ni msanii gani wa muvi unayemkubali kwa hapa Tanzania, wa kike na wa kiume?
Msanii wa kiume ninayemkubali ni Kojaki, huyu kijana anaweza kufika mbali sana lakini kwa msanii wa kike ni Monalisa.
Unazungumziaje wasanii hasa wa kike wanaoamini katika uvaaji wa nusu utupu ndani na nje ya muvi zao?
“Nawashauri waache kufanya hivyo kwa kuwa ili uwe msanii mwenye kukubalika lazima uwe na heshima ya mavazi na uwe mwenye busara ya kuwa na kauli inayofaa mbele ya watu. Kuvaa nusu utupu siyo njia ya kuwa na mafanikio hata kidogo waige mfano wa wasanii kama Natasha, Thecla Mjata na Lucy Komba wanajiheshimu sana.”
Je, kweli wasanii wa kike na wa kiume wenye sura nzuri na maumbo ya kuvutia ndiyo wanaopewa kipaumbele zaidi kwenye soko la filamu? “Kwanza kabisa ningependa watu waelewe kwamba uigizaji hautaki watu wenye muonekano mzuri peke yao, inategemea ‘script’ inasemaje, kuna sehemu anahitajika mtu asiyevutia hata kidogo lakini sehemu nyingine inamhitaji mtu anayevutia.”
Unazungumziaje uwepo wa makundi kwenye sanaa ambapo kuna kundi moja linaloonekana lina nguvu zaidi ambalo linaundwa na mastaa na lile la chini ambalo ni la wasanii wasiokuwa na majina makubwa ambalo mara nyingi limekuwa halipewi kipaumbele?
“Hilo kweli lipo na kweli makundi haya yanatutenganisha sana. Ningependa niwashauri tu wasanii tusiwe na choyo badala yake tuwe na ushirikiano na upendo.”
Unawashauri nini wasanii wanaotumia pesa zao vibaya bila kujiwekea akiba kisha baadaye kuishia kuombaomba?
“Kwa bahati nzuri siku hizi kuna mifuko kibao ya hifadhi za kijamii ambapo mtu anaweza akajiwekea akiba yake ikamsaidia uzeeni. Nawashauri wasanii wenzangu watumie pesa zao vizuri na wapunguze anasa kwani kuwa msanii hakumaanishi kila siku uende klabu na kufuja pesa na wapambe.
Hao wapambe mara nyingi hubadilika wakikuona umefulia, wasanii wajitahidi kutumia fursa ya vipato vyao kujenga waige mfano wa Masanja, AY na wengine ambao wamejiimarisha vizuri na wana mafanikio.”
Mipango yako ya baadaye katika sanaa ipoje?
Kwa sasa nafanya kazi kwa ukaribu sana na Pilipili Entertainment lakini sijafungwa kufanya kazi na kampuni nyingine. Mipango yangu ni kufanya muvi kimataifa kama vile ile muvi niliyoifanya Sri Lanka inayoitwa A Love Like This