Archive Pages Design$type=blogging

DENTI WA KIDATO CHA NNE ATEKWA, AUAWA

Stori: Haruni Sanchawa SIMANZI! Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo Kitunda, jijini Dar...

Stori: Haruni Sanchawa SIMANZI! Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo Kitunda, jijini Dar es Salaam, Enock Mseti (20) alitekwa na watu wasiojulikana kisha kuuawa kikatili na maiti yake kutupwa kando ya reli hivi karibuni. 
Mwili wa Enock Mseti ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kitunda, baba mzazi wa marehemu, Reuben Mseti alisema kijana wake ambaye hakuwa na tabia ya kushiriki katika makundi maovu, aliondoka jioni baada ya kufanya kazi zake za nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake.
“Mwanangu alikuwa afanye mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, ingawa kutokana na hali yangu kiuchumi kuwa mbaya, alikuwa amesimama kwenda shuleni, lakini nilikuwa katika jitihada za kuhakikisha anafanya mtihani huo,” alisema mzee Mseti kwa huzuni. 
Jeneza likipelekwa makabulini kwa ajili ya mazishi.
“Hili ni pigo  kubwa sana kwangu na familia yangu ndugu mwandishi, maana kijana huyu ndiye alikuwa kila kitu hapa nyumbani, ukizingatia  mimi na mke  wangu umri umeshatuacha. “Kwa jinsi mwili wake ulivyokutwa, inaonekana aliuawa mbali na pale alipotupwa kwa sababu katika paji la uso wake, kulionekana alama ya kupigwa na kitu kizito, mikono na miguu yake ilikuwa imevunjwa, lakini nguo alizovaa hazikuwa na damu kuonyesha kama kulikuwa na purukushani.
 
“Sehemu aliyokutwa marehemu ni mita chache tu kutoka nyumbani katika eneo ambalo lina kipori kidogo karibu na ilipopita reli,” alisema mzee Mseti.
Kijana ambaye ni msaidizi wa kazi za nyumbani kwa mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Seleman Abdallah alisema siku ya tukio marehemu aliondoka na kurudi nyumbani majira ya saa nne kuulizia chakula, akidai kuwa awekewe kidogo tu kwani asingekula sana, kisha akaondoka.
“Marehemua aliondoka na akarudi kama saa 5 hivi usiku na kuondoka tena, lakini safari hii hakurudi hadi tulipopata taarifa za kufa kwake  jambo ambalo lilitushangaza,” alisema Abdallah. Marehemu alizikwa katika Makaburi ya Kinyamkera yaliyopo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: DENTI WA KIDATO CHA NNE ATEKWA, AUAWA
DENTI WA KIDATO CHA NNE ATEKWA, AUAWA
http://api.ning.com:80/files/3KGM3KZVxz7xqssz79fIjacB3MHiwIygzyjb7RoaScWaOJggTxW3vjSQW87s3Cq4UuFYI2qx2fydK*HOYFB*DUAnW*7MM*kl/IMG20141108WA0052.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/denti-wa-kidato-cha-nne-atekwa-auawa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/denti-wa-kidato-cha-nne-atekwa-auawa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago