October 18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka k...
October
18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye
msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka kwenye mikoa
mbalimbali ya Tanzania.
Ilikua ni good time ya ukweli sana Watanzania kumuona T.I kumuona
Davido kumuona Victoria Kimani na Waje pamoja na wasanii wengine wa
kimataifa ambao nao walihudhuria tamasha hili lililokuwa na watazamaji
zaidi ya elfu hamsini.
Miongoni mwa wasanii waliopokelewa vizuri kwenye show hii ni pamoja
na Mr Blue na Micharazo,Ally Kiba,Weusi,Vanessa Mdee,Stamina pamoja na
Diamond Platnumz ambaye aliimba single 4 kwenye jukwaa hili.
Mashabiki wengi wa Ally Kiba inasemekana walipanga kuzomea wakati
Diamond Platnumz anaperfoam pale jukwaani,kupitia 255 ya XXL ya Clouds
Fm meneja wa Diamond Platnumz aitwae Babu Tale kaongelea hali hii.
Hizi ni sentensi 10 alizozisema.
1.Sisi tumechukulia sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na
uongozi wa Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili
tukaitwa tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na
kumwambia kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate
Diamond kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu
kama ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga
kelele kwa ajili yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi
unaenda wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu
tumpigie kura Diamond kwenye tuzo za Channel O Music Awards, kwa sababu
mwisho wa siku chema chajiuza kibaya chajitembeza.