Staa wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa skendo ya kujihusisha ya vitendo vya kisagaji i...
Staa wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa
skendo ya kujihusisha ya vitendo vya kisagaji inayomuandama
imemsababishia msala mkubwa kwa mama yake na kuamua kumuomba radhi.
Akizungumza na Global publisher, Aunty Lulu alisema mama yake ana
ugonjwa wa presha hivyo amejirekebisha katika eneo hilo ili asiweze
kumkwaza tena mzazi wake huyo.
“Najua nimemuumiza sana mama yangu, nachukua fursa hii kumuomba sana
samahani kwa kuwa najua aliumia sana kutokana na habari hiyo lakini
nataka kumuambia kuwa mimi mtoto na nitaendelea kuwa mwanaye, anisamehe
mama yangu,” alisema Aunty Lulu.