Recho Kizunguzungu amesema hana desturi ya kuandika nyimbo zake kabla ya kuingia studio. Amesema nyimbo nzuri huziandika anapopata mzuka ...
Recho Kizunguzungu amesema hana desturi ya kuandika nyimbo zake 
kabla ya kuingia studio. Amesema nyimbo nzuri huziandika anapopata mzuka
 kutoka kwa producer.
“Kiukweli nyimbo zangu nyingi huwa siandiki yaani huwa inatokea 
studio hapo hapo, huwa napenda kuingia studio na kuanza kufanya kazi. 
Muziki ujue ni mood mtu hawezi akakuamsha asubuhi akakuambia uende 
studio, na usifanye kitu chochote ukiwa hauna mzuka huwezi kufanya kitu”
 Recho aliiambia Bomba FM ya Mbeya.
Kwa upande mwingine Recho alisema kujitambua kwake ndio njia kuu 
inayomfanya asiteteleke katika muziki kutokana na kuutegemea zaidi 
katika kupata kipato cha kuendeshea maisha yake. “Siri kubwa nikujua ni 
kitu gani unakifanya, kwa sababu kuna mtu mwingine anakuwa anafanya 
halafu hajui kitu gani anakifanya, yaani hajielewi yuko wapi? Mimi 
ninafanya muziki halafu muziki ndio maisha yangu.”




