post-feature-image
HomeBurudani

MAMA YAKE AMTUPA, KISA MGONJWA

MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika. ...

NEW TRACK:- BOB JUNIOR & ROMA - MAUMIVU
NDOA YA JIDE, GARDNER AFUNGUKA - JISOMEE HAPA
DIAMOND AMPIGA VIJEMBE WEMA SEPETU - SOMA UTAMBUE ALICHOMWAMBIA WAZI WAZI
MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika.
Habari zinasema mtoto huyo baada ya kuokotwa alifikishwa katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala ambako alipokelewa na kulelewa.
Mtoto Sauda Mohamed aliyeokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake.
ALIVYOOKOTWA
Sauda aliokotwa na msamaria mwema maeneo ya Buguruni sehemu ya wazi akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye hajafahamika.
Chanzo chetu kilisema mara baada ya kuokotwa taratibu zilifanyika kwa kumfikisha Kituo cha Polisi Buguruni kisha akapelekwa moja kwa moja katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo, Dar.
Akifafanua kuhusu tukio hilo mkurugenzi wa kituo hicho, Mwanaisha Magambo alikuwa na haya ya kusema: “Sauda aliokotwa akiwa na umri wa miaka mitatu hata hivyo, walifanya vipimo vya kitaalamu ili kujua umri kwa kumpima kichwa na baadhi ya viungo vya mwili wake.
“Alipookotwa alikuwa na hali mbaya sana kipindi hicho kwani alilazwa mwezi mzima katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapumlia mashine na mapigo ya moyo yalikuwa juu sana.
AGUNDULIKA MATUNDU KATIKA MOYO
“Kutokana na kuwa na hali mbaya, madaktari pale Muhimbili baada ya vipimo wakagundua kuwa ana matundu mawili kwenye moyo wake.
“Baada ya kugundulika tatizo alipewa dawa za kutumia na akaruhusiwa lakini hali ilibadilika na ikalazimu arudishwe tena Muhimbili ambako amelazwa.”
Mtoto Sauda Mohamed akiwa amelala.
MAANDALIZI YA SAFARI YA INDIA
Magambo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo Sauda hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea, akitaka kusogea huwa anatambaa.“Mbaya zaidi ugonjwa huo umemfanya Sauda asiwe na uwezo wa kusema na mwili wake umedhoofu ikiwemo miguu.
“Kuna maandalizi yanafanywa ili apelekwe India kwa matibabu zaidi kutokana na ukweli kwamba tatizo lake ni kubwa maana sasa hata kula hawezi,” alisema.
  Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, mlezi wa mtoto huyo, Bi. Magambo alisema amefariki dunia na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar.
WITO KWA WAZAZI
Tunapenda kutoa wito kwa wazazi kwamba si vema kutupa watoto. Matatizo ya Sauda yalichangiwa kutokana na kutupwa na mzazi wake, hivyo kukumbwa na maradhi lukuki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina- Mhariri.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MAMA YAKE AMTUPA, KISA MGONJWA
MAMA YAKE AMTUPA, KISA MGONJWA
http://api.ning.com:80/files/YkTQKvQouurP8VapDA3wRCieITatHbjkgBAdxXB-TrZoPpnz0t1sCffOvEPO-q72odXOYgglT8Chr1pvq69s5lFECtzM0dDl/TOTO2.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/mama-yake-amtupa-kisa-mgonjwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/mama-yake-amtupa-kisa-mgonjwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago