Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa mara nyingine t...
Kesi
ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa
kalenda kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu
anayeendesha kesi hiyo kupata shughuli nyingine nje ya
ofisi.Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya
ya Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo
mwendesha mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo
kutokana na Hakimu Williberforce Luwhego kupata dharura.
Kesi
hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu
ambapo Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande
wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne kwenye kesi hii
inayomkabili mume wa Flora Mbasha anaekabiliwa na
mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara
ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha
alikwenda Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu
wake na hakukutana wala kuongea na mume wake ambapo muda
mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.





