Dakika kadhaa baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanza...
Dakika
kadhaa baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika
kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz
aliekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu wake.
‘Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima
hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi
tulipo leo, katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40
kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni
kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante
sana kwa wote wanaozidi kunisupport’