Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na M...
Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea
kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na
Meninah Atick.
Diamond ameiambia Bongo5 kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.
“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema
msanii huyo. “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya
rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua
kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua
utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana
huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond.
“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao
vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina mahusiano na
Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi wangu,
ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara.
Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu
hawawezi kumchukia! Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa
watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”
“Unajua kitendo hicho hatamaye kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi
wake halafu anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu
hakimpendezi. Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia
njia hiyo. Labda wana wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii
tutaweza kuamharibia Diamond. Ndioa siku zote nimekuwa kimya tu ila sina
mahusiano na Meninah. Mie nikiwa na mtu huwa sifichi naweka wazi
kabisa. Hata kama leo nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche? Mie
katika mambo yangu huwa simuogopi mtu kama ningekuwa nataka kuoa basi
ninge weka wazi why nifiche?”