Jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa muimbaji wa ‘Jikubali’, Ben Pol kwakuwa pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, mpenzi wake amb...
Jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa muimbaji wa ‘Jikubali’, Ben
Pol kwakuwa pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, mpenzi wake
ambaye huenda ndiye aliyemuimbia wimbo wake mpya ‘Twaendana’, Latifa
Mohamed alimwandikia ujumbe mtamu na kuweka wazi uhusiano wao.
Latifa ambaye alishika nafasi ya pili kwenye shindano la Miss
Tanzania 2013, pia alijumuika na mpenzi wake huyo katika kitengo cha MOI
kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kutoa misaada kwa watoto
wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Kupitia Instagram, Latifa ameandika kuwa Ben Pol ni mwanaume anayempa furaha.
“On this special day napenda kumshukuru Mungu,mama na baba kwa
kukuleta duniani. Umekua ni mtu muhimu sio kwangu tu bali kwa
familia,marafiki,na waTanzania kwa ujumla. Mwanaume
mkarimu,mnyenyekevu,muelewa,mcheshi,mwenye upendo,moyo wa
dhahabu,mtanashati,busara #Handsome_With_Brains ninayemfahamu,”
ameandika Latifa.
“Thank you kuwa muongozo kwangu,wadogo zako na mtu yoyote..We ni
mfano wa kuigwa, Mungu azidi kukubariki na akuongezee mengi Benard.
Ntaandika mengi sana lakini yote hayawezi kuisha Mungu tu ndo anaeyajua
niliyo nayo na alitukutanisha kwa sababu.. HAPPY BIRTHDAY rafiki
yangu,muongozo wangu,msiri wangu, pacha wangu,mtu unipae furaha kila cku
#Mzaziiii. Have a blast #firstborn @iambenpol #SUPER_MAN #HERO.”