Baada ya gazeti la Amani leo (August 21) kuandika story inayomhusisha Diamond na biashara ya madawa ya kulevya,...
Baada ya gazeti la Amani leo (August 21) kuandika story
inayomhusisha Diamond na biashara ya madawa ya kulevya, meneja wa msanii
huyo Babu Tale amekanusha taarifa hizo na kudai muziki anaofanya
Diamond unalipa kuliko madawa.
Akizungumza leo, Babu Tale amesema pesa anayoingiza Diamond kupitia muziki ni nyingi kulipo pesa ya madawa.
“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya,” amesema Tale.
“We get more money from music, sio kwenye madawa ya kulevya,
hatufanyi hizo biashara na kama wanahisi sisi tunafanya tunawaruhusu
watufanyie investigation hata kwa muda wa miaka kumi ina maana
tunavyopita pale airport hawana vifaa vya kutuchunguza? Ipo wazi hata
Global walishindwa kufanya kazi na sisi kwa sababu sisi ni wakubwa. Sasa
leo hii tunauza madawa ya kulevya kwa sababu tunakomaa kwenye bei zetu.
September tunafanya show kubwa ya Unplugged na msanii wa kwanza hapa
kufanya ile show ni Diamond na ile show hawalipi hela ya kis**e,
wataendelea kuona watu wanauza madawa ya kulevya, hakuna msanii wa
Tanzania anayefanya show kwa walau dola elfu 10,000 ni Diamond peke yake
wengine ni dola elfu 2000, 2500 elfu 3,000 mwisho. Tuna show Marekani
show kumi na tano (15) show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa
Tanzania hatufanyi show chini ya dola elfu 15,000,” ameongeza Tale.