MUME wa mtu na baba wa watoto watatu, Tito Onesmo Machibya amekiri kuzaa watoto wawili na mfanyakazi wake wa ndani ‘hausigeli’ akidai ...
MUME
wa mtu na baba wa watoto watatu, Tito Onesmo Machibya amekiri kuzaa
watoto wawili na mfanyakazi wake wa ndani ‘hausigeli’ akidai kuwa
amefanya hivyo kwa vile ni msaidizi wa mkewe katika ndoa.
Akizungumza na waandishi wetu jijini Dar mwanzoni mwa wiki hii, Tito
alisema imani yake ya Kikristo inamwambia kuwa mwanamke haruhusiwi kuwa
na wivu na kama anataka ndoa yake idumu basi ni vema mwanaume awe na
uhusiano wa kimapenzi na msaidizi wa kazi za ndani ya nyumba.
“Mama kama unataka ndoa yako idumu na mume wako akupende sana basi
kama una hausigeli jitahidi umkabidhi mumeo atembee naye na wivu
hauruhusiwi, hapo ndoa itadumu,” alisema Tito.
Mwanaume huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa mke wake hana wivu hivyo amekubali kwa moyo mweupe yeye kuzaa na hausigeli huyo na wanaishi nyumba moja.
Mwanaume huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa mke wake hana wivu hivyo amekubali kwa moyo mweupe yeye kuzaa na hausigeli huyo na wanaishi nyumba moja.
“Kwa mujibu wa Biblia, hausigeli ni mjakazi, mke wangu nimezaa naye
watoto watatu na hausigeli watoto wawili, wote tunaishi nyumba moja
kasoro vyumba na mimi ndiyo naamua leo nakwenda kulala na nani,”
alisema.
“Nawashauri wanaume wenzangu watembee na mahusigeli wao maana ukiwa
na hausigeli na hujatembea naye ni dhambi kubwa sana. Mfano mzuri ni
Ibrahim (mume wa Sarah) wa kwenye Biblia alizaa na hausigeli wake,
Hajiri (mtoto Ishmaili), Yakobo naye alizaa na mtu na dada yake (Leah na
Raheri).”
Tito akaongeza: “Hausigeli hatakiwi kutamaniwa na mtu yeyote wa nje
kwa sababu Biblia inasema hausigeli ni kitanda cha baba na ikitokea mtu
mwingine wa nje ya mimi akamtamani hausigeli wangu nitatoa laana.”