Hapa ni kwenye gari safari ya kuelekea studio ndio inaanza, Mameneja Bab Tale kushoto na Salam kulia pembeni na Diamond Hatimae mpang...
Hapa ni kwenye gari safari ya kuelekea studio ndio inaanza, Mameneja Bab Tale kushoto na Salam kulia pembeni na Diamond
Hatimae mpango wa Mafikizolo wa South Africa ambao ni mastaa wa hit
single ya ‘khona’ waliochukua tuzo mbili kwenye MTV Africa music awards
2014 kufanya kolabo na Diamond umefanikiwa kwenye usiku wa June 9 2014.
Diamond pamoja na mameneja wake wawili ambao ni Salam na Bab Tale
waliongozana mpaka kwenye studio za msanii mkongwe aitwae Oskido ili
kurekodi kolabo hiyo ya Mafikizolo, kundi la Afrika kusini lililorudi
kwenye chati kupitia mikono ya Oskido.
Ndio tunawasili kwa Oskido, mtu wako wa nguvu nilikuepo kuhakikisha kila kinachotokea kinakufikia
Kama hukusikiliza Clouds FM Top 20 Jumapili ya June 8 2014, wakati wa
kufanya mazoezi ya tukio la MTV kwenye tuzo za Mama Durban South Africa
June 7 2014, Mafikizolo waliomba kurekodi wimbo na Diamond baada ya
kushawishika kufanya nae kolabo hivyo wakaahidi kushughulikia gharama
zote za kumuongezea Diamond muda wa kuendelea kukaa South Africa pamoja
na kubadili ticket ya ndege ili wakamilishe kazi yao.