MKONGWE wa Bongo Fleva na mwanachama wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama ambaye ni mchumba wa aliyekuwa Miss Ruvuma miaka ya nyuma, I...
MKONGWE
wa Bongo Fleva na mwanachama wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama
ambaye ni mchumba wa aliyekuwa Miss Ruvuma miaka ya nyuma, Isabela
Mpanda, amekiri kuwa bibie huyo ni msalaba wake, hivyo hata amkosee
kiasi gani, hatamuacha.
Aliyekuwa Miss Ruvuma miaka ya nyuma, Isabela Mpanda akipozi.
Mkongwe wa Bongo Fleva na mwanachama wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama.
Maisha ya wawili hao kimapenzi yamekuwa ya kutatanisha hasa kutokana
na kuachana na kurudiana kila mara, kitu ambacho Karama anasema
kitafikia mwisho kwani furaha yake ni kuona anafunga ndoa na mpenzi wake
huyo wa muda mrefu
“Mimi nimeshakubali kuwa Bela ni msalaba
wangu na ndiyo maana hata kama ananikosea vipi au mimi namkosea,
tunaweka mambo sawa na maisha yanaendelea kama kawaida,” alisema Karama
ambaye mshirika wake, Inspekta Haroun, juzikati aliadhimisha miaka kumi
ya ndoa yake.