post-feature-image
HomeBurudani

HUYU NDIO MREMBO ALIYECHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU

INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso...

VURUGU UJERUMANI, KUKAMATWA PROMOTA SIRI 7 ZAFICHUKA SHOO YA DIAMOND
UKIWA HODARI WA KUHONGA, KAA MKAO WA KUACHWA WAKATI WOWOTE!
DENTI ANAYEDAIWA KUPIGWA NA DIWANI HOI HOSPITALINI!
INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed.
Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi, mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na vicheko vyao, akahisi wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa Stella, kumbe alikuwa na kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja wa majirani wa wanawake hao.
Wasamaria wema walimpeleka Stella Kituo cha Polisi Tegeta ambapo ilifunguliwa kesi nambari TGT/RB/1969/2014 - Kujeruhi kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa nyuzi 19 usoni na nane kifuani.

Stella akiuguza majeraha.
Akizungumza kwa tabu nyumbani kwake, Stella alisema: “Amenionea tu, hapa sijisikii vizuri. Nahisi kizunguzungu na giza kila ninaposimama, pia siwezi kula vizuri chakula kwani kila ninapotafuna, kichwa kinaniuma sana.”
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: HUYU NDIO MREMBO ALIYECHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU
HUYU NDIO MREMBO ALIYECHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU
http://api.ning.com:80/files/uxLbwSVx3LvLCEmSTQIoJCDfoiKZT5z-SiTEPth9XiXNidag4o41bC4f8fh90vNEUfcUu4Hu4Th0ItNkuDVmTe6fiUDEafmh/CopyofIMG_0246.JPG?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/05/huyu-ndio-mrembo-aliyechanwa-na-viwembe.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/05/huyu-ndio-mrembo-aliyechanwa-na-viwembe.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago