Mwishoni mwa mwaka jana 2013 rapper Nikki Wa Pili aliwahi kusema “Namuomba Mungu anipe PHD nikiwa Kijana”, na hatimaye ndoto hizo zinaen...
Mwishoni mwa mwaka jana 2013 rapper Nikki Wa Pili aliwahi kusema
“Namuomba Mungu anipe PHD nikiwa Kijana”, na hatimaye ndoto hizo
zinaenda kutimia.(Ingia hapa)
Nickson Simon anayefahamika kwa jina la kisanii Nikki Wa Pili ambaye
pia ni msemaji wa kundi la Weusi, amesema leo kuwa ameamua
kurudi chuo kwaajili ya kusoma PHD in Development studies baada ya kuona
ana muda mwingi unaopotea.
“Kilichonisukuma ni kwamba yaani sasa hivi 100% nafanya muziki, na navyokuwa nafanya muziki hauandiki nyimbo kila saa hauendi studio kila saa, unafanya muziki wakati una mood. Sasa kama kijana nimeona natumia muda mwingi sana nakaa gheto naangalia movie, nikaona huu muda naweza nikafanya kitu kingine ambacho kwangu naona ni productive(…) kwahivyo nikaona kukaa tu hivyo muda unapotea bure unajua muda una thamani sana”.

Nikki amesema tayari ameshaanza kufanya taratibu za usajili na wiki ijayo ataanza kuingia darasani.
“Yaani hapa navyoongea na wewe naenda kumalizia registration, masomo tutaanza wiki ijayo, wiki hii tutaanza orientation UDSM.”
Rapper huyo wa ‘Sitaki Kazi’ ambaye mwaka jana alihitimu shahada yake
ya pili ya Uzamili katika Maendeleo (Masters) chuo kikuu cha Dar es
salaam, ameelezea malengo yake atakapohitimu PHD.
“Malengo yangu ni kwamba kuna hivi vitu vyangu ambavyo navifanya binafsi nataka baadae vije viwe vikubwa, kama hii taasisi yangu Twaonekana nataka ije iwe kubwa, na pia nikienda shule inaniongezea confidence, naweza kwenda nikaongea na watu wengi wakaniamini. Nataka kufanya biashara, na baadae sana kama nitafikiria kufanya kazi labda nitahitaji kuwa mwalimu wa chuo.”