ZIKIWA zimepita saa takriban sita tangu kuzikwa kwa msanii mahiri wa nyimbo za...
ZIKIWA zimepita saa takriban sita tangu kuzikwa kwa msanii
mahiri wa nyimbo za Kwaya, Kapteni John Komba, anayetajwa kuwa karibu
zaidi na wasanii wa fani zote, Mchekeshaji Steve Mengere ‘Steve Nyerere’
alifanya bonge la pati la kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ndani ya Hoteli
ya JB Belmont iliyopo katikati ya Jiji la Mwanza, usiku wa Jumanne
iliyopita.
Katika pati hiyo ambayo waalikwa walikula na kunywa, mke wa
mchekeshaji huyo aitwaye Zawadi ndiye alikuwa kivutio kwani watu wengi
hawakutegemea kama Steve ameoa ‘kifaa’.
“Dah, hapa Steve ndiyo kamaliza mchezo kabisa, huwezi kuamini kama
anaweza kuwa na mke mzuri namna hii, hapa amewapiga bao mastaa wenzake,”
alisikika akisema muigizaji mmoja wa kike anayefanya kazi jijini Mwanza
aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy.
Hata hivyo, katika sherehe hiyo kulikuwa na idadi kubwa ya wageni
waliojitokeza wakiwemo mastaa kama vile Jacob Steven ‘JB’, Single
Mtambalike ‘Rich’ na wengineo ambao walikuwa marafiki wa marehemu
Kapteni Komba.
Ijumaa lilifanya jitihada za kuongea na Steve ili kujua sababu
za kufanya pati hiyo wakati msiba wa Kapteni Komba ukiwa bado ‘mbichi’
bila mafanikio lakini rafiki yake aliyedai si msemaji wa msanii huyo
alisem walikuwa jijini Mwanza kikazi hivyo hawakuweza kuhudhuria mazishi
ya Komba ndiyo maana Steve aliamua kufanya kitu katika kuadhimisha siku
yake ya kuzaliwa.