post-feature-image
HomeBurudani

HUYU NDIO MCHUNGAJI ANAYEDAIWA KUTELEKEZA MKE

Mchungaji wa kanisa analosali msanii wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ na wenzake lililopo Sinza, Dar, Godwin Mwamposa amekanyaga ...

Video:- Msanii wa Kenya atumia tshs milioni 12 kukodi helikopta kuhudhuria hafla za mwanae na mdogo wake, Nairobi na Eldoret kwa siku 1
Birthday party ya Diamond imegharimu Tsh milioni 28, na zawadi ya BMW X6 imenunuliwa M 90
HIZI NDIO PICHA ZA AWALI ZA KILICHOJIRI KWENYE BIRTHDAY YA DIAMOND - ZIANGALIE HAPA
Mchungaji wa kanisa analosali msanii wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ na wenzake lililopo Sinza, Dar, Godwin Mwamposa amekanyaga skendo kufuatia madai ya kumtelekeza mkewe aitwaye Sylvia mwenye mtoto mmoja ambayo imetua kwenye dawati la gazeti hili.
Mchungaji Godwin Mwamposa na mkewe siku ya ndoa yao.
Ndugu wa Sylvia afunguka
Awali, ndugu aliyejitambulisha kuwa anaishi na Sylvia (jina tunalihifadhi kwa sababu maalum) alisema mke wa mchungaji huyo kwa sasa anaishi maisha magumu maeneo ya Buza jijini Dar baada ya kuachwa kwenye mataa na mwenza wake huyo.
“Yaani mpaka nimeamua kuwaambia hii habari nimeona ndugu yangu anateseka sana, tena na mtoto wake ambaye amekuwa akimuulizia baba yake kila siku.
“Mgogoro ulianza siku nyingi wakiwa Moshi (Kilimanjaro) ambapo Mchungaji Mwamposa alimwambia Sylvia wanakuja Dar kwa ajili ya kutoa huduma lakini walipofika alimpeleka kwa wazazi wake Buza (Dar) na kumuacha huko.“Kuna wakati wazazi wa Sylvia walimuita lakini alichenga kwenda, hali iliyosababisha sintofahamu kwa wanandugu.
“Sylvia analia kila siku, mara ya mwisho alipata presha ya kushuka na kulazwa Muhimbili (Hospitali ya Taifa) mpaka akawekewa mashine ya kupumulia kwani alikuwa na hali mbaya lakini pamoja na hilo bado mchungaji huyo hakusogea wala kuulizia hali yake,” alisema ndugu huyo.
Wakiwa na nyuso za furaha siku ya ndoa yao.
Ilidaiwa kwamba, kutokana na mazingira hayo, wanandoa hao waliofunga ndoa mwaka 2008 huko Kilimanjaro kwenye Kanisa la Calvary Assemblies of God, walikwenda kwenye usuluhishi katika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo Morogoro lakini mambo hayakuweza kutengamaa.
Mke atafutwa
Baada ya kupata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Sylvia na kuzungumza naye juu ya madai hayo ya kutelekezwa ambapo alikiri kuwepo tatizo lakini akasema asingependa kuliongelea kwa sababu hakuwa na hali nzuri.
“Samahani sitaweza kulizungumzia sana suala hilo kwani sipo vizuri,” alisema Sylvia na kuomba apewe muda.
Mtoto wa mchungaji naye anenaBaada ya kuzungumza na Sylvia, mtoto wa mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la Angelprincess alizungumzia mazingira magumu anayoishi kutokana na kuwa mbali na baba yake.
“Natamani kumuona baba yangu, naishi mazingira magumu na mama yangu. Yaani siku nikimuona baba nitafurahi sana,” alisema mtoto huyo.Mchungaji Mwamposa anasemaje?
Hii ni shahada ya ndoa yao.
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, mchungaji Mwamposa alionesha kuwapo kwa tatizo kati yake na mkewe na akaeleza kuwa, suala lao lipo kwenye uongozi wa juu wa kanisa lake.
“Kama mnaweza kumsaidia msaidieni lakini suala hili lipo kwa uongozi wa juu wa kanisa na mkitaka zaidi mtafuteni wakili wangu muongee naye.”
Licha ya kiongozi huyo wa dini kumpatia mwandishi namba ya simu anayotumia mwanasheria huyo, ilipopigwa iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa meseji hakujibu hadi tunakwenda mtamboni.
Gazeti hili linaendelea kufuatilia habari hii kwa karibu na chochote kitakachopatikana, utakisoma kwenye Magazeti ya Global
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: HUYU NDIO MCHUNGAJI ANAYEDAIWA KUTELEKEZA MKE
HUYU NDIO MCHUNGAJI ANAYEDAIWA KUTELEKEZA MKE
http://api.ning.com:80/files/KhhA6XZToLoiTKYnp383VDs2aUFgkBBn1MW3y0MeaQMDIstqBN7wczXUOGGR3OBNHZfUTsu0hsl5mYCQcb6sMGWeRnkre3tt/IMG20150318WA0041.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2015/03/huyu-ndio-mchungaji-anayedaiwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2015/03/huyu-ndio-mchungaji-anayedaiwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago