post-feature-image
HomeBurudani

MUME, MCHEPUKO WAGOMBEA MTOTO, mKE ADAI KUTEMBEA NA WOTE WAWILI SIKU MOJA

Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuaw...

MWANAFUNZI WA CHUO DODOMA AFYATUA ZA UCHI NA KUZIRUSHA MTANDAONI
JUA SABABU TANO ZA KUKAUKA KWA UKE WAKATI WA KUFANYA MAPENZI
Nimezikuta Twitter Muda Huu - Nimeshindwa Kuelewa Kulikoni? Labda Wadau Lakini #MashujaaPoolParty2014

Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.
Mwanamke, Bahati Ramadhani anayeidaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko.
Tukio hilo la kushangaza lililojaza kadamnasi lilijiri nyumbani kwa wakwe hao, Mtaa wa Mawenzi jirani na Soko la Matunda la Mawenzi la mjini hapa wiki iliyopita ambapo Bahati alikuwa akiishi na mumewe, ldd Yusuf.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.
Polisi akimbana kwa maswali mwanamke huyo kuhusu utata uliotokea.
Siku ya tukio, mama mkwe wa Bahati, Faidha Cosmas alishtukia dili baada ya kuona sms ya mwanaume ‘aliyeseviwa’ kwa jina la Saddy kwenye simu ya Bahati ikimweleza kwamba alikuwa amemtumia fedha za matumizi ya mtoto wao huyo.
Baada ya mama mkwe kuona ishu hiyo alimwambia mwanaye Idd ambapo kwa pamoja walimpigia Saddy aliyekiri kuwa anachojua mtoto huyo ni wake na amekuwa akituma fedha za matumizi.
Mama mkwe alisema kwamba walimwita Bahati na kumuuliza kama anamfahamu Saddy ambapo alikiri kuchepuka.

Mwanamke, Bahati Ramadhani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Baada ya mzozo wa hapa na pale, mawifi wa Bahati waliingilia kati na kuibua bonge la mtiti wakimpa wifi yao kipigo hadi mwandishi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio.
Alipofika mahali hapo na kuona hali ya hatari ndipo akaita polisi wa doria ambao walifika na kutuliza ghasia.

Familia hiyo ilishuhudiwa ikiwa kwenye kikao ambapo uamuzi wa awali ulikuwa ni ldd kumuacha mara moja Bahati.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo kwenye eneo la tukio.
Hata hivyo, katika uamuzi huo wa awali, Bahati alikubali kuondoka lakini kwa masharti ya kuondoka na mwanaye jambo ambalo liliikera familia hiyo na kumvamia wakitishia kumtoa roho.
Kabla ya mambo kuwa mabaya, polisi wakiongozwa na Afande Mwajabu waliingilia kati na kumuokoa Bahati.

Afande Mwajabu aliwahoji wahusika na baada ya maelezo, ldd alitoa uthibitisho wa kadi ya kliniki ambayo ilionesha yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.
Katikati ni mtoto anayegombewa katika utata uliojitokeza.
Mwandishi wetu pamoja na Afande Mwajabu walimpigia simu Saddy ambaye kwa sasa yuko masomoni mkoani lringa na kuweka ‘loud speaker’ ambapo alipoulizwa alisema:
“Mtoto ni wangu. Kwa sasa ana umri wa miaka 2 na kadi ya kliniki ninayo.”
Saddy alipoulizwa na mwandishi wetu kwa kipindi chote cha miaka miwili, mtoto wake alikuwa akiishi wapi alisema:

Mwanamke aliyegonganisha wanaume akichepuka akichukuliwa na mapolisi kutoka eneo la tukio.
“Nilikuwa bize na masomo lakini najua mwanangu yuko na mama yake.”
Kwa upande wake, Idd ambaye ndiye anayeishi na Bahati (huku akitokwa machozi) alisema hakutarajia kama mkewe angemsaliti kiasi hicho.
Bahati alipohojiwa, alisema kuwa siku aliyopata ujauzito alitembea na Saddy pamoja na mumewe ldd hivyo hata yeye anashindwa kujua baba halali wa mtoto wake.
Sakata hilo lilifikishwa polisi ambapo bado linatafutiwa suluhu.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MUME, MCHEPUKO WAGOMBEA MTOTO, mKE ADAI KUTEMBEA NA WOTE WAWILI SIKU MOJA
MUME, MCHEPUKO WAGOMBEA MTOTO, mKE ADAI KUTEMBEA NA WOTE WAWILI SIKU MOJA
http://api.ning.com:80/files/RjUGj58MiaFA3deAUQmNcpfKE4u-Mbnf3YgVh15w33ZnE03bmwu9ytRWoQp0vGjQixiWZk98RknhcXT6s-ATWkq1eFmsaqhw/IMG_7385.JPG?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2015/01/mume-mchepuko-wagombea-mtoto-mke-adai.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2015/01/mume-mchepuko-wagombea-mtoto-mke-adai.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago