WAKATI staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akitafutwa kufanya kolabo na w...
WAKATI
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akitafutwa kufanya kolabo
na wasanii mbalimbali, nyota wa muziki huo kutoka Moro Town, Dayana
Nyange, ‘Dayna’ ameibuka na kusema hana mpango wa kufanya kazi na staa
huyo hata kama anafanya vizuri kimataifa.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Kwa kweli sijapaga kufanya kazi na msanii huyo na kwangu sitazami
eti anafanya vizuri nje na mimi nimpe kazi yangu hapana, nataka msanii
ambaye anaweza kusimama kwenye ngoma yangu, bila hivyo bora nifanye
mwenyewe,” alisema Dayna.
Nyota wa muziki huo kutoka Moro Town, Dayana Nyange, ‘Dayna’.
Akifunguka na Risasi Vibes, Dayna alisema kuwa hajaweka wazo la kumpa
kolabo staa huyo kwani hajui kama kuna kazi ambayo anaweza kufanya
vizuri ikiwa pindi atakapo mshirikisha, ingawa wapo ambao wanahitaji
kufanya naye kazi.