Archive Pages Design$type=blogging

PATCHOU MWAMBA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUMANIWA

Muonekano wa Patchou Mwamba ‘Tajiri’ baada ya kupata uvimbe usoni. Vunja ukimya! Mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokr...



Muonekano wa Patchou Mwamba ‘Tajiri’ baada ya kupata uvimbe usoni.

Vunja ukimya! Mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ya Bongo, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ ameibuka na kufungukia skendo ya kufumaniwa iliyosambaa kwa kasi kama moto wa kifuu.


‘Mzee wa Ngwasuma’, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ akiwa ndani ya Ofisi za Global.

Wikiendi iliyopita, uvumi wa Patchou kufumaniwa uliibuka na kusambaa mitandaoni kufuatia kuwepo kwa picha iliyomuonesha akiwa amevimba usoni hususan katika maeneo ya macho na mdomoni.
Watu mbalimbali mitandaoni, walitumiana picha hiyo huku wakisindikiza na ujumbe wa mtu aliyeiposti awali na kuandika kuwa mwanamuziki huyo amevimba baada ya kufumaniwa na kutembezewa kichapo cha mbwa mwitu.

Wakati Ijumaa Wikienda likiwa katika harakati ya kuchimba ukweli wa jambo hilo (kawaida ya Global Publishers), mwanamuziki huyo alitinga katika ofisi za gazeti hili na kutumia dakika 30 kuanika ukweli kuhusiana na uvumi huo.

“Nimesikitishwa sana na jambo hili. Sijafumaniwa chochote, watu tu wameamua kunichafua. Mimi nina ‘aleji’ na pombe, kuna dawa nilishauriwa niwe nakunywa kila ninapotaka kunywa pombe.

“Sasa bahati mbaya siku hiyo nikalazimisha kunywa bila kutumia dawa, uso ndiyo ukavimba namna ile. Sasa nilijipiga picha usoni nikaposti Instagram na kuwaomba watu ushauri kama wanajua tiba ya ugonjwa wangu wanisaidie, nikashangaa ghafla watu wakaisambaza picha hiyo na vichwa vyao tofautitofauti, imenisumbua sana,” alisema Patchou huku uso wake ukiwa umerudi katika hali yake ya kawaida.

Mhariri-Kuna kila sababu ya serikali kupitia Wizara ya Sayansi na Teknolojia kulitazama kwa jicho la tatu suala la watu wanaokurupuka na kuposti picha sizizokuwa na ukweli au ukiukwaji wa maadili maana tatizo hili linazidi kushamiri kwa sasa.
CHANZO; GPL

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: PATCHOU MWAMBA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUMANIWA
PATCHOU MWAMBA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUMANIWA
http://api.ning.com/files/kdMiOwfaxveVNJ4KmSntj*5qo8S7g93Oap*sc9daXepK0mguSxs4SaDh6vxPIfZiI70Y9cCKLCicUNhIUuywCWheW5lybbve/pacho_mwambaaa.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/patchou-mwamba-afungukia-ishu-ya.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/patchou-mwamba-afungukia-ishu-ya.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago