Archive Pages Design$type=blogging

MASTAA WANUSA KIFO AJALI YA NDEGE!

Mastaa kutoka tasnia ya uigizaji Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Isaya Mwakil...

Mastaa kutoka tasnia ya uigizaji Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Alex Chalamila ‘Mac Regan’, Sekioni David ‘Seki’ na abiria kibao wamenusurika kufa katika ajali ya ndege.
 
Abiria wakiingia ndani ya ndege.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tukio hilo lilijiri asubuhi ya Alhamisi iliyopita uwanjani ambapo ndege waliyopanda ya Shirika la Ndege la Fastjet aina ya FN 141 Airbus ilipata hitilafu kwenye injini ya kushoto ilipokuwa ikiruka. Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili muda mfupi baada ya tukio hilo baya, Dude alisimulia mkasa huo kwamba, ndege hiyo ilikuwa kwenye spidi ikipaa angani ndipo ikafeli na kuanguka. Dude alisema taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kwamba kabla ya kuruka, ndege aina ya kunguru aliingia kwenye injini ya kushoto na ndiye aliyesababisha hitilafu hiyo kisha ndege ikakosa mwelekeo na kuserereka chini.
 
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Alisema wakati inaserereka ilikwenda kutua kwenye majani ambapo waliokolewa na fire (zimamoto).
Baada ya abiria hao kuokolewa, waliwekwa kwenye chumba maalum kutokana na baadhi yao kutaharuki na kupandwa na presha.
“Tunamshukuru Mungu tumepona maana ajali ilikuwa mbaya sana.
“Tulikuwa tunaenda Mwanza kisha mimi nitaenda Bukoba na akina Masanja wataelekea Mara kwa shughuli za kisanaa.
 
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’.
“Hapa mimi niko sawa ila wenzangu hawajiwezi kwa presha,” alisema Dude.
Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa wasanii hao na abiria wengine walipatiwa ndege nyingine wakaendelea na safari.
Juhudi za kumpata msemaji wa Fastjet, Lucy Mbogoro ili azungumzie ajali hiyo hazikuzaa matunda baada ya simu zote, ya ofisini na kiganjani kuita bila kupokelewa.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MASTAA WANUSA KIFO AJALI YA NDEGE!
MASTAA WANUSA KIFO AJALI YA NDEGE!
http://api.ning.com:80/files/u-nuBgwJg3zQGjpnDuqyQzbuqr6wT1eRNjkHiWNdZ465KTYU0yBc5NjdyLwWqupXV*Bf*ZeYJP8VEPLUnBI4Hc98oXrqG8dV/fastjet.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/mastaa-wanusa-kifo-ajali-ya-ndege.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/mastaa-wanusa-kifo-ajali-ya-ndege.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago