La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda k...
La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.
La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.
MWANADADA, aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother
Hotshots, Irene Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza
na Idris wameondoa gundu kwa ushindi wao.
Akizungumza na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda
kuungana na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,
“Binafsi nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani
300,000, ni furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia
Diamond kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi
kutoka Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa
gundu kwa wasanii wa Kitanzania’, alisema.
Aidha La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris
siku atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika
ramani nzuri kimataifa.