Archive Pages Design$type=blogging

KUMBE KUMWAGWA ALIANZA ZAMANI

KATIKA historia hii ya maisha ya Diamond, wiki iliyopita tuliishia pale ambapo Diam...

KATIKA historia hii ya maisha ya Diamond, wiki iliyopita tuliishia pale ambapo Diamond alikuwa amemwagwa na demu wake kisa kikiwa msichana huyo kutovumilia maisha duni ya msanii huyo. Tunaendelea…
Mkali wa miondoko ya Bongo Fleva 'Diamond Platnumz' akiwa mbele.
Diamond anakwenda mbele zaidi kwa kukumbuka maneno makali na yenye kuchoma moyoni ambayo aliambiwa na demu huyo ambapo kila akiyakumbuka hata leo, bado haamini kilichotokea!
NI MANENO YENYE KUCHOMA
“Nakumbuka siku hiyo yule demu aliniambia, ’sikiza Diamond, mi’ kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana masilahi kwangu.’

Neno ‘mwanaume ambaye hana masilahi kwangu lilimuumiza nyota huyo kwani aligundua kumbe ulimwenguni ili upate vitu vizuri ni lazima uwe na fedha kwa vile yeye hakuwa na ‘mpunga’, demu alimtoka hivihivi anajiona.
AKUTANA NA MDHAMINI MWINGINE
Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Platnamuz au ‘Sukari ya Warembo’ anasema mwaka 2009, alikutana na  Peter Msafiri ‘Papaa Misifa’ ambaye alisema atamsaidia kumkuza kisanii mpaka atoke na kuwa tishio Bongo.

Diamond anasema akiwa na Papa Misifa alifanikiwa kurekodi Wimbo wa Nenda Kamwambie. Anasema:
“Huu wimbo nilimtungia Sarah, mpenzi wangu aliyenimwaga kwa sababu sikuwa na masilahi kwake (hivi karibuni amemwagwa na Wema Sepetu).“Nilimweleza kwenye wimbo ni kwa kiasi gani niliumia kwa kuniacha kwake wakati nilikuwa bado nampenda.”

'Diamond Platnumz' na kikosi chake wakiwa kazini.
AANZA KUNG’ARA, ANUNUA GARI
Diamond anakiri kwamba, alianza kung’ara katika sanaa na wimbo huo na maisha yakabadilika kiasi cha kufika hatua ya kununua gari la kwanza kabisa aina ya Toyota Celica.

ALBAMU YA KWANZA
Februari 14, 2010, Diamond aliachia albamu yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo kumi. Nyimbo hizo ni Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Nalia na Mengi, Binadamu, Nakupa, Usisahau, Uko Tayari, Wakunesanesa, Toka Mwanzo na Jisachi.Anasema Aprili mwaka huohuo alikuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kushinda tuzo 3 za Tanzania Kili Music Awards.

Anazitaja tuzo hizo kuwa ni ya Msanii Bora Chipukizi, Wimbo Bora wa Mwaka (Kamwabie) na Wimbo Bora wa R&B (Kamwambie). Kama vile haitoshi, heshima ikapanda kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Malaria Tanzania.
HILI PIA ANALIKUMBUKA
Diamond anasema Wimbo wa Mbagala ulipendwa sana kwani mwaka huohuo ukiwa unavuma sana, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete ‘JK’ alimteua kuwa mburudishaji kwenye ziara za kampeni ya Uchaguzi Mkuu Rais, mwaka 2010 ambapo JK aliibuka kidedea.

Itaendelea wiki ijayo.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: KUMBE KUMWAGWA ALIANZA ZAMANI
KUMBE KUMWAGWA ALIANZA ZAMANI
http://api.ning.com:80/files/3pbaBKayUO*kpB5arQ3f8Eb087qDZzg9glv2I3etI0eXMZB2bHBsLsRpNbBp0RfKXy5ao6QVZEptAoBKUURR*tTeb00MlvqK/damon.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/kumbe-kumwagwa-alianza-zamani.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/kumbe-kumwagwa-alianza-zamani.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago