Stori: Mayasa Mariwata LEGENDARY wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ amesema ...
Stori: Mayasa Mariwata
LEGENDARY wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ amesema kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo vimemkalia kushoto ni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe, yeye siku zote hufanyia kanisani kwa kufanya maombi.
“Watu wanashindwa kuelewa tu, kinachopaswa kufanywa ni kumuomba Mungu akuzidishie maisha marefu ikibidi kutoa sadaka na siyo kuandaa shughuli kubwa ambayo mwisho wa siku yanafanyika mambo ya ajabu ya kumchukiza Mungu, mimi huwa naenda kanisani ni sherehe tosha na kumbukumbu zangu zinaonyesha ni siku moja tu ukubwani kwangu ilikuwa mwaka juzi nilifanyiwa bethidei na wasanii wa Bongo Movie kwa kunishtukiza,” alisema JB.