Katika safu hii wiki hii tunaye mwanadada anayeyaendesha maisha yake kwa kuuza su...
Katika
safu hii wiki hii tunaye mwanadada anayeyaendesha maisha yake kwa kuuza
sura kwenye filamu Bongo. Huyu si mwingine bali ni Eshe Buheti.
Kama ilivyo ada naye aliwekwa mtukati na mwandishi wetu Imelda Mtema
na kuulizwa maswali ambayo alitoa ushirikiano katika kuyajibu.Ijumaa:
Unaonekana kutoandamwa na skendo kama inavyokuwa kwa mastaa wengine, hii
inatokana na nini?
Eshe: Unajua mimi ni mke wa mtu, najichunga sana kuhakikisha
sichafuki kwa namna yoyote, ndiyo maana unaona skendo zinanipitia mbali.
Ijumaa: Hebu tuambie, unapokuwa nyumbani unapendelea kuvaa mavazi gani?
Eshe: Nikiwa ndani kwangu hasa na mume wangu akiwepo ni mwendo wa khanga moja kwa kwenda mbele.
Eshe: Nikiwa ndani kwangu hasa na mume wangu akiwepo ni mwendo wa khanga moja kwa kwenda mbele.
Ijumaa: Mastaa mbalimbali inakuwa vigumu kuolewa na wakiolewa hawadumu kwenye ndoa zao, wewe unadhani utadumu?
Eshe: Kila jambo anapanga Mungu, kikubwa najitahidi kumheshimu mume
wangu na kumfanyia kila linalomfurahisha na kuacha yanayomkera, naamini
kwa kufanya hivyo ndoa yetu itadumu.
Ijumaa: Najua una mtoto mmoja sasa, vipi una mpango wa kuongeza mwingine soon?
Ijumaa: Najua una mtoto mmoja sasa, vipi una mpango wa kuongeza mwingine soon?
Eshe: Mwanangu anaonesha kabisa anataka mdogo wake, kwa hiyo
tunajipanga na naamimi hatuna muda mrefu tutafanya maandalizi ya kumleta
kiumbe mwingine duniani.
Ijumaa: Wanaume wengi hawapendi kazi ya usanii hasa kutokana na
skendo mbalimbali, vipi wewe mume wako amewezaje kukubaliana na kazi
yako?
Eshe: Nahisi mume wangu ni mtu wa tofauti, ananiamini na kwa kuwa hajawahi kusikia lolote baya, wala hana wasiwasi.
Eshe: Nahisi mume wangu ni mtu wa tofauti, ananiamini na kwa kuwa hajawahi kusikia lolote baya, wala hana wasiwasi.
Ijumaa: Kuna mastaa ambao wana katabia ka’ kuiba waume za watu, siku ukijua kuna anayemnyemelea mumeo utafanyaje?
Eshe: Huyo atakuwa ananitafuta shari na kwa kweli ajiandae kwa mpambano. Siwezi kuingiliwa kwenye anga zangu halafu nione sawa tu.
Eshe: Huyo atakuwa ananitafuta shari na kwa kweli ajiandae kwa mpambano. Siwezi kuingiliwa kwenye anga zangu halafu nione sawa tu.
Ijumaa: Kutokana na tabia ya mastaa wengi kuwa na kucha ndefu na
kutopenda kiziharibu hata kupika hawawezi, wewe kwako hili likoje?
Eshe: Kwa mambo ya mahanjumati yani hapa ndiyo umefika, omba siku nikualike uje kula kwangu ndiyo utajua mimi ni mpishi au mbabaishaji.
Eshe: Kwa mambo ya mahanjumati yani hapa ndiyo umefika, omba siku nikualike uje kula kwangu ndiyo utajua mimi ni mpishi au mbabaishaji.
Ijumaa: Ni mambo gani ambayo huyapendi kabisa kwenye maisha yako?
Eshe: Mimi sipendi umbeya, uvivu, majungu kwani ni vitu ambavyo vinaturudisha nyuma.
Eshe: Mimi sipendi umbeya, uvivu, majungu kwani ni vitu ambavyo vinaturudisha nyuma.
Ijumaa: Kwenye sanaa kuna vishawishi vingi sana hasa hii tabia ya
baadhi ya maprodyuza kupenda sana rushwa ya ngono, wewe unakabiliana
vipi na changamoto hiyo?
Eshe: Najitambua na ninajiheshimu sana. Siwezi kujivunjia heshima yangu kwa mambo ya kijinga kwa hiyo Mungu ananisaidia navuka changamoto hizo.
Eshe: Najitambua na ninajiheshimu sana. Siwezi kujivunjia heshima yangu kwa mambo ya kijinga kwa hiyo Mungu ananisaidia navuka changamoto hizo.
Ijumaa: Unawashauri vipi hawa mastaa ambao mabifu ni sehemu ya maisha yao?
Eshe: Hili ni tatizo na kwa kweli ni vyema sisi mastaa tukawa na umoja na tukashirikiana katika kuendeleza sanaa yetu badala ya kugombana.
Eshe: Hili ni tatizo na kwa kweli ni vyema sisi mastaa tukawa na umoja na tukashirikiana katika kuendeleza sanaa yetu badala ya kugombana.