post-feature-image
HomeBurudani

DIAMOND MCHAWI...

Stori: Waandishi Wetu NYOTA yake inang’ara hata mchana, siku hadi siku anazidi kuwa...

Stori: Waandishi Wetu NYOTA yake inang’ara hata mchana, siku hadi siku anazidi kuwa wa kimataifa zaidi. Awali walisema anang’aa kwa sababu ana uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania, 2006, Wema Sepetu lakini juzikati wamemwagana, jamaa bado yuko juu! Watu wanauliza, ni mchawi?
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifurahia tuzo alizojinyakulia huko Sauzi.
Huyu si mwingine ni nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye juzi alitua nchini akitokea Afrika Kusini ‘Sauz’ alikoshinda tuzo 3 za Channel O zilizofanyika jijini Johannesburg nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Diamond alilakiwa na maelfu ya mashabiki wake ambao wengi walikuwa wakihoji kung’aa kwake kunatokana na nini!
“Jamani watu ni wengi sana, mimi nataka kuwaambia huyu Diamond si ajabu anatumia uchawi.

Mimi natokea Sinza Mori jirani na kwa mama yake Diamond, sijala hadi muda huu (saa 8:25) lakini sina njaa nataka tu kumwona Diamond,” alisikika akisema mmoja wa mashabiki waliofurika uwanjani hapo.
Mwingine alisema inawezekana Diamond akawa anatumia ‘kizizi’ kwani hakuna Mbongo Fleva aliyeng’aa kwa muda mrefu kama yeye na kila siku anazidi kwenda juu badala ya kushuka.

...Mamia ya mashabiki wakimshangilia staa huyo.
ALIVYOTUA
Baada ya Diamond kuwasili, msafara wa kutoka uwanjani kuelekea mjini ulianza ambapo alipitia Buguruni- Chama. Alipofika hapo Diamond alishuka kwenye gari na kutembea kwa miguu kitendo kilichowafurahisha mashabiki wake kumwona msela ‘anapiga maguu’.

“Huyu ndiyo shujaa wetu wa kweli, hata kama wengine wanasema kuwa si nguvu za kawaida zinazomuweka juu lakini jamaa anajua kujituma,” alisikika mmoja wa mashabiki waliofurika Buguruni.
WAELEKEA MAGOMENI
Baada ya kumalizana na watu wa Buguruni, Diamond akiwa amezungukwa na umati, aliendelea kutembea kwa miguu hadi  Ilala-Mchikichini, akapanda bodaboda kuelekea Kariakoo huku gari lake likimfuata kwa nyuma.

Umati wa watu ukimsindikiza mkali huyo.
Mapaparazi wetu waliendelea kuufatilia msafara huo ambao ulitikisa jiji kutokana na idadi kubwa ya watu kuguswa na kuufuata kiasi ambacho ilibidi polisi waingilie kati.“Afadhali polisi wameingilia kati maana pengine watu wangeweza kuuana le hapa,” alisema Juma Dodi, mkazi wa Kariakoo.
POLISI WAMVUSHA
Kuonesha kwamba wanajali, Polisi wa Kituo cha Msimbazi jijini Dar, walilazimika kumvusha nyota huyo kutoka Kariakoo kwa kutumia ‘difenda’ lao hadi maeneo ya Jangwani wakamuacha aendelee na msafara wake kwa kutumia gari lake aina ya Toyota Prado.

WAELEKEA TANDALE
Msafara huo ulioambatana na bodaboda, magari mengi ya wadau wa muziki Bongo, ulielekea moja kwa moja nyumbani kwao Tandale na kukaa kwa muda mfupi huku kila mtu ‘Diamond Diamond huku watu waliotarajiwa kupiga buu (Timu Wema) wakiingia mitini.

Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Baada ya hapo, msafara ukaanza tena kuaelekea ukumbi maarufu wa burudani ya Escape One uliopo  Mikocheni jijini Dar kwa ajili ya mkutano maalum na waandishi wa habari.
Diamond alishinda tuzo hizo akiwa ameshindana na wasanii kibao kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: DIAMOND MCHAWI...
DIAMOND MCHAWI...
http://api.ning.com:80/files/R5SqbRTCmAHxFBuUC0Q7Nyg2TJB6PHZckmPlQas0aeABemVNT-*6qOUytU1ILKhRQxogEpyYTKjDvnRIKx8KisGyikKwpbuH/DIAMOND.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/diamond-mchawi.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/diamond-mchawi.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago