Na Mwandishi Wetu BAADA ya kuona filamu zinazidi kuwa za kihuni, msanii wa siku n...
Na Mwandishi Wetu BAADA
ya kuona filamu zinazidi kuwa za kihuni, msanii wa siku nyingi kwenye
tasnia ya filamu Bongo, Tumaini Alfred ‘Aunt Fifi’ ameamua kugeukia
upako na hadi sasa ameshawaombea watu mbalimbali wenye ukimwi, viziwi na
kupona kabisa.
Aliyekuwa msanii wa Filamu Bongo, Tumaini Alfred ‘Aunt Fifi’.
Akizungumza na Amani, Aunt Fifi alisema amekuwa akipita nyumba hadi
nyumba kwa ajili ya kufanya huduma hiyo ambayo hadi sasa zaidi watu 30
wamepata huduma yake na kupona kabisa.“Awali nilipenda kutoa upako lakini nilikuja kusita baada ya kuingia kwenye filamu, na wakati huo nikiamini kuwa filamu zinalipa, baada ya kuona hakuna jambo jipya, nimeona bora nirudi kwenye nguvu zangu za kuponya watu,” alisema Fifi.
Fifi alipata kutamba katika filamu mbalimbali zikiwemo Copy, Sound of Death, Senior Bachelor, I Deserve It, Kaburi la Mapenzi, Fake Smile, Daddy, Cross My Sin na nyinginezo.