STAA mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika atarejea kwa Mwen...
STAA mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo
Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika
atarejea kwa Mwenyezi Mungu lakini kwa sasa bado anakula ujana.
Staa mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’.
Akipiga
stori na Ijumaa Wikienda, Amanda alisema kwa sasa umri wake unamruhusu
kula ujana kwa mambo ya starehe kama kuvaa mavazi ya kuacha mwili wake
nusu utupu kwa sababu muda wa kurejea kwa Mungu bado haujafika.
Amanda akipozi.
“Jamani
niacheni na mavazi yangu, ukifika muda nitarejea naona mnanisema sana,
kama wewe Mungu amekujalia kusali, mshukuru mimi muda huo bado
haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo alikuwa ametupia kivazi
kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake hasa tumboni.