MSANII nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amenaswa katika picha akiwa na mzungu anayeonekana kumzidi umri...
MSANII nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi
maarufu kama Amanda, amenaswa katika picha akiwa na mzungu anayeonekana
kumzidi umri ambaye unaweza kumwita kijeba aliyemtambulisha kama rafiki
yake.
Msanii nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akiwa na mzungu.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema, picha hizo ziliibwa
katika simu ya msanii huyo na mtu asiyefahamika, ambaye kwa lengo
lisiloeleweka, alianza kuzitawanya kwa watu mbalimbali.
Inadaiwa kuwa Amanda amekuwa akionekana
sehemu tofautitofauti jijini Dar akiwa na mzungu huyo ambaye anasemekana
kuwa na makazi yake maeneo ya Masaki.Amanda alionekana kushtushwa baada
ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa picha hizo na kukiri kuwa ni kweli mtu
huyo anafahamiana naye.
Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akipozi.
“Duh! hizo picha zimefikaje kwenu? Jamani haya ni maisha yangu
binafsi naombeni mniache na huyo jamaa ni rafiki yangu sana, kwanza siyo
mtanzania ni raia wa Uturuki,” alisema muigizaji huyo