Archive Pages Design$type=blogging

SITTI MTEMVU KUVUA LA TEMEKE, CHANG’OMBE

HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo v...

HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji  mwingine wakimtaka avue mataji mengine mawili.

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.
Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.
Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli amedanganya, anajijua.
“Kama angekuwa hajadanganya, kwa nini asitoe paspoti yake inayomwonesha ana umri wa miaka 23? Mambo yalimfika shingoni ndiyo maana. Anachotakiwa ni kuvua taji la Miss Chang’ombe na Miss Temeke mwaka huu,” alisema Ismail Chandu, mkazi wa Temeke jijini Dar.
 
Shindano la kumsaka Miss Chang’ombe lilifanyika Juni 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Dar ambapo Sitti aliibuka kidedea akifuatiwa na Paulina Elisante (anayetakiwa kuchukua taji), wa tatu ni Derena David.
Shindano la Miss Temeke 2014 lilifanyika Agosti 22,  mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe jijini Dar ambapo Sitti Mtemvu aliibuka kidedea akifuatiwa na Salama Saleh (anayetakiwa kushika nafasi ya kwanza) na nafasi ya tatu ilitwaliwa na Neema Mollely.
Novemba 5, mwaka huu, Sitti Mtemvu aliiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake kuvua taji hilo.Sitti alifikia uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo ya kudanganya umri wakati akigombea taji hilo.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: SITTI MTEMVU KUVUA LA TEMEKE, CHANG’OMBE
SITTI MTEMVU KUVUA LA TEMEKE, CHANG’OMBE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9orYoky5f0UpSXyEwdyc-wQU09U8dOZ2VWKrndmLK4zHa-KDzufcbKqBAZGbLMOD09OX_YN6lluGnwoc5eMnuM7rUI5l2X3ubWWOAJJgjZCEetC4kldB2XAHH4onXITGpFWf8pXaHaMQ/s1600/SITTI2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9orYoky5f0UpSXyEwdyc-wQU09U8dOZ2VWKrndmLK4zHa-KDzufcbKqBAZGbLMOD09OX_YN6lluGnwoc5eMnuM7rUI5l2X3ubWWOAJJgjZCEetC4kldB2XAHH4onXITGpFWf8pXaHaMQ/s72-c/SITTI2.JPG
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/sitti-mtemvu-kuvua-la-temeke-changombe.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/sitti-mtemvu-kuvua-la-temeke-changombe.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago