MSANII anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa kwa kipindi kifupi ambacho ameza...
MSANII
anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina Omary
‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa kwa kipindi kifupi ambacho amezama kwenye
penzi la staa wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, amempa
mahaba mazito kiasi cha kumfanya asimkumbuke aliyekuwa mkewe.
‘Sabby Angel’ akipozi.
“Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye mapenzi kama huyu na mimi
zawadi nitakayompa ni mapenzi mazito na nitamaliza ufundi wangu wote
kwake na kamwe hatokumbuka kama aliwahi kuwa na mke kabla yangu,”
alisema Sabby.Bob Junior aliwahi kumuoa mwigizaji, Halima Ally kisha
wakamwagana baada ya kuzaa naye mtoto mmoja.
Msanii wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi na 'Bob Junior' kimahaba.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Sabby alisema kuwa ameamua kuonyesha
ufundi wake wote wa kimahabati kwa msanii huyo kwani ni mwanaume ambaye
amemuona mwenye mapenzi ya dhati.