Imekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila ai...
Imekua
stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye
familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo
cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.
Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi
kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show
aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea
baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko
nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM
inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo
sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu
yake ya kukamatwa Airport.
Kuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>>
‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake…
tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji,
tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema
nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona
mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote
tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda
wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na
maisha yangu kama kawaida’
Kuhusu kukamatwa Aiport
na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba
natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo
lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua
nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa
kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam
kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na
nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu
nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo,
imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati
kushoto… sio kama nimeficha au nini’
‘Sio
kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe
nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi
nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona
akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi
pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na
nimeitoa mwenyewe’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia
bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama
mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na
hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.