MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwana...
MAMA
wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora
Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwanaye basi
asali sana.
Mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akifunguka mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama Kanumba
alisema pengo la mwanaye katika sanaa linaonekana wazi hivyo ni vyema
kwa anayetaka kuliziba kufuata nyayo zake.
”Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu, kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.
Marehemu Steven Kanumba,enzi za uhai wake.
“Tatizo wasanii wetu hawa hawapendi kuthubutu wamekalia tu kufanyiana
majungu, hawapendi kuona mwenzao anafanikiwa wanaanza kumfitini, ni
vizuri wangejifunza kitu kwa Kanumba ambaye alipenda kuthubutu,” alisema
mama Kanumba.
”Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu, kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.