HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muhar...
HALI
tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam,
Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa
gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake
zimeanza kuchunguzwa.
Mfanyabiashara
maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama
Chonji(mwenye suti), akiwa chini ya ulinzi.
Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali
zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja
na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi
maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza
kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo.Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.
Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na
Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa
na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote
wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike.