Waumini waliovalia nguo fupi watimuliwa kanisani Waumini wa kanisa katoliki la St. Francis mjini Diani kusini mwa pwani ...
Waumini waliovalia nguo fupi watimuliwa kanisani
Waumini
wa kanisa katoliki la St. Francis mjini Diani kusini mwa pwani ya Kenya
walipigwa na butwaa baada ya baadhi yao kuzuiwa kuingia katika kanisa
hilo kutokana na mavazi yao yaliokuwa nusu uchi.
Julia
baraza ambaye alikuwa amevalia kisibao ,ukanda wa manjano na viatu
vyenye kisigino kirefu alishangazwa na sheria hizo mpya ambazo
zilimsababisha kukosa misa ya asaubuhi.
Kulingana
na gazeti la the standard nchini kenya,Julia alisema kuwa watu wawili
walimsimamisha nje ya mlango wa kanisa hilo na kumwambia kwamba mtindo
wake wa mavazi ulipigwa marufuku katika kanisa hilo na kwamba ametakiwa
kuvaa mavazi ya heshima.
Aidha wasichana waliokuwa wamevalia suruali walilazimishwa kujifunga leso juu yake.
Julia alisema kwamba iwapo makanisa yataanza kufuata sheria kama hizo basi wengi hawatahudhuria maombi.
Baadhi ya
waumini wamesema kuwa mhubiri wa kanisa hilo aliyejulikana kama Joseph
pekee alikuwa ametangaza katika ibada ya awali kwamba mavazi yasio ya
heshima hayatakubalika katika kanisa hilo.
Chanzo:BBC