Mwanamitindo, mtangazaji wa TV na msanii wa muziki na filamu Jokate Mwegelo ameingia tena ndani ya stu...
Mwanamitindo, mtangazaji wa TV na msanii wa muziki na filamu
Jokate Mwegelo ameingia tena ndani ya studio za Pesa Records chini ya
producer Allonem na kuandaa wimbo mpya uliopo kwenye hatua za mwisho.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni producer wa studio hiyo Allonem,
alisema Jokate amebadilika na kuimba nyimbo za Kiswahili na kudai
amebadilika kutoka kwenye uimbaji wa kutumia Kiingereza zaidi.
“Jokate tumefanya naye kazi mbili, moja imeshatoka ni ile ambayo
ali-perform kwenye show ya Fiesta Mwanza na baada ya hapo tukakaa chini
na kuandaa wimbo mpya ambapo mpaka sasa hivi upo katika hatua za
mwisho,” amesema producer huyo.
“Sema Jokate sasa hivi yuko mbio sana ila akitulia itamalizika. Pia
studio ya Pesa Record tukiwa chini ya mkurugenzi wetu Mwinyi Pesa
tumeanzisha Pesa Entertainment ambayo ina msanii Becka Title. Atatoa
wimbo ijumaa hii itakuwa kama ndo kama anatuzindulia licha ya kuwa kuna
mambo mengine yatafuata,” aliongeza Allonem ambaye pia alitengeneza beat
ya wimbo wa Fid Q na Bi Kidude.