Kuna mambo uwa yanatokea na yanasikitisha mpaka nikaamua kueleza hivi,pia mimi si mbaguzi i...
Kuna mambo uwa yanatokea na yanasikitisha mpaka nikaamua kueleza hivi,pia mimi si mbaguzi ila nilichokiona nikikaa kimya itakuwa mbaya zaidi.Ngoja niende kwenye mada nisiwachoshe.
Nimeshuhudia vijana wengi walioko nje na ambao wameoa mtu ambaye si mtanzania,siku akifariki analetwa yeye tu.Mke na watoto ata hawaji wanaendelea na maisha yao.
Ata ambao wanakuja wakimaliza msiba tu na kuondoka hawarudi tena Tanzania.Hii inapelekea wazazi na ndugu wa marehemu kushindwa kabisa kuwaona wajukuu wao na ndio inakuwa mwisho.
Ata wengi wanaojaribu kutaka kwenda kuwaona uishia kunyimwa Visa ubalozini kwa sababu mbalimbali.Hii inasikitisha sana familia hizo.
Pia ukioa mtu ambaye si mtanzania ujue hawezi kukuvumilia siku ukimzingua anaenda kudai talaka mahakamani na anaomba child support. Hapo ujue utakatwa mshahara wako kwa ajili ya watoto tena wanakata kubwa.
Hii inafanya watu kukimbia nje na kurudi bongo mwisho wake unaanza kuandika mada nje kubaya kama mtu mmoja umu JF ilivyomtokea na kukimbia familia unajikuta una miaka zaidi ya 50 ndio unaanza familia na kuaanza kukimbizana na mabebs wa mjin u kno uku wanakulia pesa tu .
Kuna wenzetu wa Kenya ata wa West akipata karatas lazima atamtafuta mwenzake na atamsafirisha na kumuoa.Na wanaishi vizuri sababu ya kujuana tamaduni lakin wabongo upenda sifa yuko na mzungu au mtu wa uko.Mwisho wa siku unaishia matatizoni .
Ni jukumu lako sasa kunisikiliza au kupotezea ila huo ndio ukweli niliojionea ughaibuni.