Archive Pages Design$type=blogging

DUME LANASWA LIKIMDEKEA MWANAUME MWENZAKE

KAMA kawa ni siku nyingine ambayo mapaparazi wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simb...

KAMA kawa ni siku nyingine ambayo mapaparazi wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ anayewakilisha Mji Kasoro Bahari, Haruni Sanchawa ‘Cheusi’ na Richard Bukos ‘Mpiga Picha Mkuu’ walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na Mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Saa 4:23 usiku
DUME LANASWA LIKIMDEKEA MWANAUME MWENZAKE
Mkuu akiwa ofisini kwake, anaangalia saa yake na kubaini kuwa imeshatimu saa nne usiku hivyo anaamua kumtwangia Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos aliyekuwa kwenye onesho la Super Shine Modern Taarab ndani ya kiwanja kipya cha burudani cha Good Time kilichopo Kigogo Luhanga jijini Dar.
Bukos: Naam Mkuu wangu nakupata sawia.
Makao Makuu: Haya nieleze umeshazunguka wapi na wapi mpaka muda huu?
Bukos: Mkuu wangu mpaka muda huu nimeshazunguka sehemu mbalimbali, nilianzia katika Ukumbi wa Travertine, Magomeni ambako huwa wanapiga Jahazi Modern Taarab, Mango Garden ambapo ilibidi leo wapige Malaika Musica lakini pande zote hizo hamna kitu, nimeenda Kangaroo Pale Sinza Afrika Sana ambapo ilikuwa wapige Mashujaa Musica napo hawapo yaani Ijumaa ya  leo ina gundu kweli, viwanja vyote patupu.
Makao Makuu: Sasa uko maeneo gani mida hii?
Bukos: Mkuu baada ya mizunguko yote mida hii nipo Kigogo-Luhanga kuna kiwanja kipya cha burudani kinaitwa, Good Time nimekuta Kundi la Super Shine Modern Taarab linafanya makamuzi.Makao Makuu: Duh! Kigogo nayo imeanza kuendelea, vipi kuna vituko gani hapo ambavyo umeshaviona?
Bukos: Mkuu si unajua laana mambo ya taarab, ng’ambo ya hiki kiwanja kuna midume miwili. Moja linamdengulia mwenzake kama jike, nahisi litakuwa ‘kuku mtamu’. Yaani mpaka linatia kinyaa, linamdekea kabisa mwanaume mwenzake kwelikweli, siku ya kiama hawa ndiyo watakuwa kuni jehanam.
Makao Makuu: Basi Bukos naona unaanza kuwashushia laana wakati wenzio wanaponda raha zao. Piga kazi mimi ngoja nimcheki, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ kutoka Mji Kasoro Bahari.
Saa 6:12 usiku
BENDI MAARUFU MORO YASAMBARATIKA
Makao Makuu: Haloo… Mkude Simba vipi hali ya hapo Mji Kasoro Bahari?
Shekidele: Mkuu hapa Moro ni majonzi makubwa.
Makao Makuu: Vipi tena Mkude Simba?
Shekidele: Mkuu kama unakumbuka mara nyingi nilikuwa nikiripoti kwako habari za Bendi ya B.C.G Musica ‘Waluguru Orijino’, sasa mmiliki wa hii bendi alipigwa risasi na majambazi huko Dar wiki iliyopita hivyo na bendi yake nayo leo hii ndiyo tumetangaziwa rasmi kuwa nayo imekufa.
Makao Makuu: Dah, imekosa mrithi?
Shekidele: Mkuu pengine mrithi angeweza kupatikana lakini kumetokea kutoelewana kati ya kiongozi wa bendi, Killer Boy na mke wa marehemu. Baada ya kutoelewana mke wa marehemu kafungia vyombo vya muziki na kuwaambia wanamuziki watafute pa kwenda.
Makao Makuu: Dah, kweli steringi akifa na picha linakwisha, uko wapi sasa?
Shekidele: Mkuu mimi muda si mrefu nilikuwa Ukumbi wa Chilakale ambapo bendi hii huwa inapiga lakini nimekuta ukumbi umefungwa hivyo mida hii nipo Ukumbi wa Samaki Sport ambapo Bendi ya Bikon inatumbuiza na nimewakuta wanamuziki watatu wa ile bendi nilipowauliza nao wamesema mama amefungia vyombo hivyo bendi ndiyo hakuna tena na wao ndiyo washapoteza ajira.
Makao Makuu: Poleni sana Shekidele kifo hakina huruma tumuombee marehemu apumzishwe kwa amani, ngoja mimi nimcheki, Haruni Sanchawa ‘Cheusi’
Saa 7:23 usiku
MAOFISA WA MAGEREZA WANASWA WAKIBANJUKA VITAMBI NJENJE
Makao Makuu: Halooo… Halooo… Sanchawa haya haraka eleza uko pande zipi.
Sanchawa: Mkuu hivi tunavyoongeza niko hapa Ukonga kwenye Bwalo la Maofisa wa Magereza Bendi yao iitwayo Magereza Jazz a.k.a Mkote Ngoma inarindimisha burudani.
Makao Makuu: Vipi kuna vituko gani hapo?
Sanchawa: Mkuu burudani zinaendelea na si unajua tena mida hii watu washachangamka, ukizingatia kiwanja chenyewe hiki vinywaji bei chee, kuna maofisa wa magereza wanacheza ile mbaya wamevua mashati wameacha vitambi nje halafu wanakatika hao yaani ni bonge la burudani.
Makao Makuu: Poa Sanchawa, ukimaliza waambie wenzako mkalale tukutane Jumatatu ofisini bila kuchelewa.
Sanchawa: Ok Mkuu, haina mbaya. Zimefika salamu.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: DUME LANASWA LIKIMDEKEA MWANAUME MWENZAKE
DUME LANASWA LIKIMDEKEA MWANAUME MWENZAKE
http://i.ytimg.com/vi/1ZLB9Y7lPw8/sddefault.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/dume-lanaswa-likimdekea-mwanaume.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/dume-lanaswa-likimdekea-mwanaume.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago