Na Imelda Mtema MTANGAZAJI mwenye maneno lukuki kutoka Radio Times FM, Khadija Shai...
Na Imelda Mtema MTANGAZAJI
mwenye maneno lukuki kutoka Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’
amesema kuwa endapo mtalaka wake, Ezden Jumanne akitaka kuoa yeye
atakuwa wa kwanza kutoa mchango wa harusi hiyo.
Mtangazaji kutoka Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’.
Dida akiwa na mtalaka wake, Ezden Jumanne.
“Ninachoamini mimi Ezden bado anasaka mke mwema na hiyo ni nzuri na
wala siwezi kuwa na bifu na mtu wake yeyote atakayempata, nitapenda
sana. Haya ndiyo maisha yasiyokuwa na chuki yanayotakiwa,” alisema Dida.
Dida ambaye kwa sasa yupo singo, alisema
japokuwa wameacha na Ezden, lakini hana bifu naye kwa sababu anaamini
kuwa yuko katika harakati za kutafuta mke bora hivyo haoni shida
kumchangia.