Wakali wa Hip Hop Tanzania Rashid na Fareed a.k.a Chid Benz na Fid Q wana mpango wa kurekodi album ya p...
Wakali wa Hip Hop Tanzania Rashid na Fareed a.k.a Chid Benz na Fid Q wana mpango wa kurekodi album ya pamoja.
Chid ambaye ameachia ngoma mpya wiki hii ‘Kimbiza’, ameiambia 255 ya
XXL ya Clouds Fm kuwa mpango wa kufanya album na Fid lilikuwa ni wazo
lake.
“Ni idea yangu nilikuwa nayo kabla sijatoa ngoma, sikujua kama
nitakuja kuwa busy na ngoma kwahiyo nilikuwa najua kwamba kwa kipindi
ambacho nitakuwa nimekaa nirekodi project na Fid, so imekuja imekuwa”.
“Mpaka sasa hivi sijarekodi lakini tupo kwenye project yetu ya mimi
na Fid, kwahiyo soon tutaanza kuirekodi kwasababu tulisharekodi ngoma
moja so nafikiri sasa now tunatakiwa tuingie mzigoni, so nahisi the
project itakuwa noma…”
Aliongeza,“mi najitayarisha kuingiaingia vistudio napitia
vistudio viwili vitatu hapa na pale, kwahiyo natafuta bado nahisi nikija
kupata msumari ntakuja tu kusema jamani eeh baada ya huu ni
huu…tunafanya album nzima inabidi tupige mikono tu Chid na Fid kwasababu
ni Rashid na Fareed, kwahiyo tumeamua sisi wenyewe kufanya kwasababu
kila siku tunakaa tunazungumza tunacheka tunatania kila siku tuko busy
na music lakini tunaweza tukapata nafasi tukafanya kitu so tumeamua
tufanye album tupige mikono ya ajabu.”