Gossip Cop wa nguvu, Soudy Brown leo kamuweka staa mwingine wa Bongofleva, Diamond Platnumz kwenye U Heard. Kutokana na kwamba Diamond...
Kutokana na kwamba Diamond hakuwa tayari
kuongelea chochote kuhusiana na kile Soudy alichokuwa anamuuliza,
Gossip Cop alilazimika kuzima kifaa cha kurekodi sauti ili Diamond ampe
story kamili.
Story ilikuwa inahusu Diamond na Wema
kutokana na kile kinachosemekana wameachana, majibu ya Diamond
yameonyesha hawako pamoja na kuzitaja baadhi ya sababu zilizopelekea
kutokea hilo, ikiwa ni pamoja na zawadi ya gari aina ya BMW ambalo
anadai Martin Kadinda hawezi kumpa, pamoja na safari za Wema China
ambazo anadai kuna mtu mwingine aliyekuwa anazifadhili.
Diamond hajazungumza chochote kuhusu yeye na Zari the Boss Lady.
Kuisikiliza U Heard bonyeza play hapa.