Baba mmoja ambaye jina halikupatikana mara ameshusha kichapo kwa wasanii ambao ni maprodyuza waliokuwa wakimchezesha mwanaye filamu bil...
Baba mmoja ambaye jina halikupatikana mara ameshusha kichapo kwa wasanii ambao ni maprodyuza waliokuwa wakimchezesha mwanaye filamu bila ridhaa yake.
Baba huyo akizuiwa ili asiendelee kushusha kichapo hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati, maeneo
ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar ambapo awali binti huyo ambaye ni
msanii chipukizi wa kuigiza aitwaye Jeniffer alidaiwa kupigwa mkwara na
baba yake kuwa asijishughulishe na masuala ya muvi na badala yake
ajikite kwenye masomo yake kufuatia tasnia hiyo kuhusishwa na skendo za
ngono.Ilidaiwa kwamba, Jeniffer alikaidi amri ya mzee wake huyo na kwenda kinyemela kurekodi vipande kadhaa vya muvi ya kikundi chao ambapo taarifa zilimfikia baba yake huyo na kuamua kutimba lokesheni.
Baada kushuhudia bintiye ‘akigaragazwa’ kimahaba, mzazi huyo alimvaa msanii Duma na kumshutumu kumharibia binti yake ambapo alimpa kibano pamoja na maprodyusza wenzake kabla ya kuamuliwa na wasanii wengine waliokuwepo eneo hilo.
Kwa upande wake, Duma alibaki na majeraha mgongoni ambayo hadi waandishi wetu wanafika eneo la tukio yalikuwa yakitoka damu.
Duma alipoulizwa kuhusiana na mzee huyo, alikana kumfahamu na kudai kuwa alipewa mamlaka ya kumtumia binti huyo kwenye muvi na kaka wa msichana huyo.
Imeandaliwa na Deogratius Mongela, Chande Abdallah na Denis Mtima.