Archive Pages Design$type=blogging

ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE

  KIMENUKA! Ndoa iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey (40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha k...

 KIMENUKA! Ndoa iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey (40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia ushahidi mzito uliotolewa mahakamani hapo kumridhisha Hakimu Hawa Mghuruta.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’ yenye makao makuu yake jijini Arusha ndiye aliyetajwa na mahakama hiyo kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ya Pamella ambaye alikuwa ni sekretari wa kiongozi huyo wa dini baada ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukionesha mapenzi kunaswa kwenye simu ya mwanamke huyo ukitokea kwa Geor Davie.
Askofu  Geor Davie akiwa na wasaidizi wake.
Ushahidi uliotolewa na mwanaume ulidai kuwa mgogoro wa ndoa yake ulitokana na mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Askofu Geor Davie.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo Namba 01 ya mwaka 2012, Hakimu Mghuruta alisema kabla ya hukumu, mahakama ilizingatia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mlalamikaji.Mke wa mtu Pamella Geofrey (katikati) anayedaiwa kutoka kimapenzi na boss wake, Askofu George David ‘Geor Davie’.
Alimtaja mtoto wa kwanza wa wanandoa hao, Sifael Wiston (15) kwamba naye aliieleza mahakama hiyo namna mama yake alivyokuwa akizini nje ya ndoa kwa kukutana na Geor Davie ndani ya gari lake lenye rangi ya silva wakati wa usiku baba yake akiwa safarini.
Mtoto huyo alianika kwamba, walikuwa wakipelekewa juisi na bajia ndani ya gari hilo lenye pazia kisha wao kufunga vioo kwa muda mrefu huku likionekana kutikisika, ushahidi ambao uliwashangaza waumini wa kanisa la askofu huyo.
Askofu George David ‘Geor Davie’ akitoa huduma ya maombezi kwa waumini.
Wiston ambaye alikuwa msaidizi wa Geor Davie, alifungua kesi ya kudai talaka kwa Pamella ili kufikia ukomo wa shauri hilo ambalo lilianza kusikilizwa na Baraza la Usuluhishi wa Ndoa mwaka 2007 lakini ilishindikana kwa vile mkewe alipeleka sababu za uongo kuwa alikuwa akinyanyaswa hivyo kuikimbia nyumba.
Hakimu Mghuruta ameamuru mali zote yakiwemo magari matatu, nyumba iliyopo Sakina na vitu vingine zibaki chini ya mlalamikaji lakini Pamella anaruhusiwa kwenda kuwasalimia watoto wake. Hata hivyo, mahakama ilimtaka Pamella kutowarubuni watoto hao kiasi cha kuathiri masomo yao

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE
ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE
http://api.ning.com:80/files/Y7WxhNqXbMaCEl*UzOx4saT*znafRkOo70yzQvfC*N8e5NUr9f0goPhSzKgdZAsMuuomHOLM6OCED9wdZM9dT4loz04u24Lw/photo1.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/askofu-geor-davie-avunja-ndoa-ya.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/askofu-geor-davie-avunja-ndoa-ya.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago