Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa...
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya
itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa
muhimu kuhusu afya kwa siku 30 mfululizo bila malipo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mwili Mzima wa Binadamu,Meshack
Shimwela(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)wakati wa kuzindua huduma mpya ya”Simu Dokta”itakayowawezesha
wateja wanaotumia mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom kupata huduma
hiyo bure jinsi ya kujiunga mteja anatakiwa kutuma neno DAKTARI kwenda
namba 15542 na Katikati ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa
Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na
watoto,Sulende Kubhoja
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
inayojulikana kama Simu Dokta, Dk Meshack Shimwela ambaye ni Bingwa wa
magonjwa ya mwili wa binadamu alisema upatikanaji wa taarifa sahihi za
kiafya ni moja kati ya hatua muhimu za kupambana na magonjwa mbali
mbali.
Dk Shimwela alisema huduma hiyo itatoa mchango mkubwa katika
kuuhabarisha umma juu ya masuala muhimu ya kiafya na kuongeza kuwa
ujumbe wa mara kwa mara utawakumbusha watu na namna ya kujikinga pamoja
na kuchukua hatua sahihi juu ya magonjwa. Shimwela aliipongeza kampuni
ya Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo kwa ajili ya umma na kusema kuwa
inaendena na Malengo ya Milenia haswa namba sita linalosisitiza
kupambana na maogonjwa mbali mbali akiwataka Watanzania kuitumia huduma
hiyo ambayo ni muhimu kwa kila mtu.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa alisema taarifa hizo zitakuwa katika mfumo wa
ujumbe mfupi wa maneno (sms) na mteja atakuwa akizipata kila siku
kupitia simu yake ya mkononi bure kwa mwezi baada ya kujisajili kwa
kutuma neno DAKTARI kwenda 15542.
“Lengo la huduma hii ni kuchochea na kusaidia wananchi kujua mambo
mbalimbali ya kiafya ambayo wamekuwa hawayajui au kuwa na taarifa zisizo
sahihi. Taarifa hizo zitakuwa zikiandaliwa na madaktari bingwa nchini
wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii.
Huduma hii itakuwa ya msaada mkubwa kwa wananchi kwani itaongeza
ufahamu wa mambo mbalimbali ya kiafya na hivyo kusaidia ustawi wa jamii
kwa kuwa na jamii yenye uelewa mkubwa wa mambo ya afya na kusaidia
kuokoa maisha ya watu wengi. Hii itakuwa ni huduma ya kwanza ya aina
yake kutolewa na Vodacom ikiwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa
mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii ambayo inahitaji taarifa
kila siku za kuwasaidia kujiepusha na maradhi au kutoa ahueni kwa
magonjwa yanayowasumbua.,” alisema
Madaktari hao na taaluma za kwenye mabano ni pamoja na Dk. Meshack
Shimwela (Bingwa wa Mwili wa Mwanadamu, Physician) Dk. Sulende Kubhoja
(Bingwa wa watoto na moyo (Paediatrician & Cardiologist)). Dk.
Munawar Kaguta, (Bingwa magonjwa ya wanawake /wajawazito
(OBST/Gynecologist)