Mu hali gani Mashosti zangu? Leo nimekuja kivingine tofauti na mlivyonizoea, sitaki kumchambua mtu, mtoto wa kike japo bila kumpasha md...
Waswahili wanasema raha ya ngoma kupokezana, siyo kung’ang’ania
kuimba peke yako. Leo nimemkaribisha mgeni ambaye ni mtu wangu wa karibu
hana tofauti na bata mzoefu wa kupata.
Leo mzungumzaji mkuu sijui nimwite shangingi wa kiume au kidume cha mbegu maana naye yumo katika kukimbizana na watoto wadogo, afadhali mwenzake nimepumua.
Leo mzungumzaji mkuu sijui nimwite shangingi wa kiume au kidume cha mbegu maana naye yumo katika kukimbizana na watoto wadogo, afadhali mwenzake nimepumua.
Nimekuwa nikijitahidi kuuzungumzia upande wa pili katika medani ya
mahaba kuhusu chakula cha nafsi lakini wapo wahusika wakuu ambao hawana
tofauti na nyani mzee aliyepanda miti mingi. Sitaki kupoteza wakati
ngoja nimkaribishe Babu Poa, Babu Poa karibu.
“Asante Bi Nasra au maarufu Bi Naa, siwezi kukuita shangingi mstaafu
kwa vile bado unatoa huduma ndogondogo kwa wazee wenzio. Tuachane na
hayo, leo nataka nizungumzie tabia za ubabe kwa wanaume kuwanyima uhuru
wake zao kiasi cha kukidhi haja zao na kuwaacha wenzao njiani.
Katika lawama nyingi nilizozikuta kwa Bi Nasra ni kutokana na tabia za baadhi ya wanawake kuachwa njiani na waume zao. Kingine kutobadilishiwa mitindo ya kupeana mautamu.
Katika lawama nyingi nilizozikuta kwa Bi Nasra ni kutokana na tabia za baadhi ya wanawake kuachwa njiani na waume zao. Kingine kutobadilishiwa mitindo ya kupeana mautamu.
Mwanamke akimwelekeza mumewe tufanye hivi unakuwa ugomvi, anamuona
mwanamke si muaminifu, akishangaa eti amejuaje kubadili staili.Nataka
niwaeleze wanaume wenzangu kitu kimoja katika kumfurahisha mpenzio ni
kumfikisha safari yake na raha ya safari kufika si kuishia njiani.
Siku hizi unasikia mwanamke anashushiwa njiani na kufika mwenyewe kwa
miguu (kukanda kwa maji ya moto). Mimi babu poa katika pilikapilika
zangu za ujana nilikuwa siwezi kumuacha mwanamke njiani hata kama mimi
nimewahi kufika nilikuwa siridhiki, lazima nitamsindikiza mwenzangu
mpaka afike.
Uanaume si ndevu, kwani hata mbuzi anazo, bali kumkata kiu mpenzi
wako, kama kula na kuvaa vyote hivyo alikuwa akivipata kwao. Lakini kuna
kitu amekifuata kwako na si kingine ni bakora hata siku moja punda hafi
kwa bakora.
Hakikisha kila ukimshika hakutaje jina lako na mwisho akupe asante,
unamnyima raha unataka azipate wapi? Haya kila ukirudi na mtindo wako
mmoja kama taa ya treni. Mpe raha mtoto wa watu, jamani kila kitu mpaka
uambiwe hujui raha ya kilio ni machozi, utamlizaje bila kumtoa machozi.
Ukipanda juu ya mnazi usiteremke mpaka uhakikishe unamtupia madafu ya kutosha mpaka akuambie ametosheka.
Ukipanda juu ya mnazi usiteremke mpaka uhakikishe unamtupia madafu ya kutosha mpaka akuambie ametosheka.
Hapa kidogo nataka nitoe somo kwa wanaume wenzangu, mapenzi si
kumwaga mzigo na kuondoka, bali wote mfurahie mwenzako kwa kumfikisha na
siku zote mwenye kutia chachu ya mapenzi ni mwanaume kwa utundu wake.
Hakuna shule ya mapenzi bali wewe mwenyewe kubuni vitu vya kumfurahisha mpenzi wako.
Wako wanaojifunza kupitia kanda za wakubwa, lakini kaka mkulima mzuri haangalii eneo lilivyo muhimu kuwepo na rutuba inayostawisha mbegu. Vivyo hivyo hata katika mapenzi mkao wowote wa mpenzi wako ni mtindo wa mapenzi.

Pia kama hujui mitindo usimfikirie vibaya mkeo kwani aliokuja nao
huenda kaelekezwa na shoga zake ambao huenda ukapunguza mateso ya
kuachwa njiani kila siku. Kwa hayo machache inatosha nakurudisheni kwa
anti yenu.”
“Asante babu poa kumbe nawe una makombora mazito nina imani wamekusikia la muhimu kuyafanyia kazi.
Kwa leo inatosha tukutane wiki ijayo, ni mimi Anti yenu Nasra Shangingi Mstaafu.