THEA upo? MUME wa msanii wa filamu za Kibongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Michael Sangu ‘Mike’ amenaswa akila raha na kifaa kipya (mwana...
THEA
upo? MUME wa msanii wa filamu za Kibongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’,
Michael Sangu ‘Mike’ amenaswa akila raha na kifaa kipya (mwanadada)
ndani ya Club East 24, Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na onesho la
B Band.
Siku hiyo, Mike na mwanadada huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, walikuwa wakijiachia ukumbini hapo huku wakipata kinywaji na kushushia na mishikaki ya bata.
Baada ya washakunaku kumshuhudia Mike
akitesa na binti huyo, walianza kuizungumzia ndoa yake na Thea na
kusikika wakikumbushia ndoa yao jinsi ilivyoyumba kiasi cha wawili hao
kutengana kabla ya kurudiana.
Kufuatia tukio hilo paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Mike na kumuuliza kuhusu uhusiano wake na mrembo huyo ambapo alisema dogodogo huyo hakuwa akimjua isipokuwa alimshtukia eneo hilo na kumlazimisha amnunulie mishikaki.
“Mimi simjui wala nini nimeshangaa amenivaa ghafla anasema yeye ni shabiki wangu baada ya hapo akaanza kunilazimisha nimnunulie mishikaki na kinywaji,” alisema Mike