MSANII wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuwa, licha ya kwamba sifa ya mwanamke ni kujua...
MSANII
wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ametoa kali ya mwaka
kwa kusema kuwa, licha ya kwamba sifa ya mwanamke ni kujua kumpikia mume
mahanjumati, yeye hana muda wa kupika ila anajua jukumu lake ni
kumstarehesha mpenzi wake tu.
Msanii wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Vai alisema hawezi kutumia muda wake
kupika awapo nyumbani kwani kazi hiyo hufanywa na hausigeli.
“Mimi nikiwa nyumbani sipiki, mpenzi wangu akija kwangu tutanunua chakula, tutakula kisha tutaendelea na mambo yetu lakini siwezi kuingia jikoni kupika, kazi hiyo atafanya hausigeli,” alisema Vai.
“Mimi nikiwa nyumbani sipiki, mpenzi wangu akija kwangu tutanunua chakula, tutakula kisha tutaendelea na mambo yetu lakini siwezi kuingia jikoni kupika, kazi hiyo atafanya hausigeli,” alisema Vai.