Katika hali ya kushangaza hivi karibuni wanamuziki Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ na Estelina Sanga ‘Linah’, waliamua kudendeka hadharan...
Katika hali ya kushangaza hivi karibuni wanamuziki Hamisi Mwinjuma
‘MwanaFA’ na Estelina Sanga ‘Linah’, waliamua kudendeka hadharani mchana
kweupee na kuwaacha watu wamepigwa butwaa.

Wanamuziki Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ na Estelina Sanga ‘Linah’, wakidendeka jukwaani.
Tukio hilo lilitokea juzikati ndani ya Uwanja wa Namfua mjini Singida
wawili hao walipokuwa kwenye shoo ya Fiesta ambapo katika kusaka mzuka
wa mashabiki, Linah alimsogezea uso FA na bila hiyana mahaba yakachukua
nafasi.
Kufuatia tukio hilo, baada ya shoo mwandishi wetu alimfuata FA ili
kumuuliza kulikoni aliamua kufanya vile ambapo hakutoa ushirikiano ila
Linah alisema, hakuona shida kwani si jambo la ajabu sana kwake hasa
linapokuja suala la burudani.