Archive Pages Design$type=blogging

MKE: ROSE MUHANDO KANIHARIBIA NDOA

MWANAMKE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Flavian Elias ameibuka na kumlalamikia mwimba Injili ‘grade one Bongo’, Rose Muhando kwamb...

MWANAMKE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Flavian Elias ameibuka na kumlalamikia mwimba Injili ‘grade one Bongo’, Rose Muhando kwamba amemuharibia ndoa yake na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Daudi au ‘Rungu la Yesu’ kisa kikiwa ni pesa na dalili za wivu wa mapenzi.
Mwanamke anayetambulika kwa jina la Flavian Elias anyemlalamikia Rose muhando kumharibia ndoa.
KISA KILIPOANZIA
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili nyumbani kwake Boko, Dar, Flavian alisema yeye na mumewe walidunduliza pesa hadi kufikisha shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya familia.
Alisema wakiwa kwenye harakati hizo, siku moja mumewe aliporudi nyumbani alimwambia Rose ana shida hivyo anaomba akopeshwe shilingi milioni moja, angeirejesha baada ya siku saba.

“Kwa kuwa mume wangu anafanya kazi na Rose (msemaji wa Rose), nilimkubalia nikiamini kwamba  fedha hiyo ingerudishwa.
“Baada ya wiki moja kupita, mambo yakawa tofauti, pesa haikurudi na mpaka ninavyozungumza na nyinyi bado haijarudi.”

ROSE HAPOKEI SIMU
“Ili kuipata pesa yangu niliamua kumpigia simu, ikawa ahadi tu, mara leo mara kesho na siku nyingine aliniambia yupo nchini Sudan ya Kusini.

Mume wa Flavian Elias, Daudi au ‘Rungu la Yesu’ .
“Sasa hali imekuwa tofauti, nikimpigia hapokei simu yangu tena.”
MAISHA YAWA MAGUMU
“Maisha yangu yamekuwa magumu, vifaa vyote vya ujenzi nimeshanunua, vipo ndani hiyo shilingi milioni moja ilikuwa ni kwa ajili ya fundi na kununua mbao za kupaulia.
“Na kwa sababu mume wangu ndiye anajuana na huyo Rose, nimemwambia asirudi nyumbani hadi aniletee hiyo fedha.

“Rose amenivurugia ndoa yangu, naishi na watoto wangu na ni muda mrefu, mume wangu anaishi huko Mbezi-Mwisho (Dar) maana mimi sitaki mchezo kabisa,” alisema Flavian, mama wa watoto wanne, wakiwemo mapacha.
DAUDI ANASEMAJE?
Baada ya madai hayo, waandishi wetu walimtafuta Daudi ili kumsikia anasemaje kuhusu madai ya mkewe.

Familia ya Flavian Elias.
“Kiukweli kabisa sikujua kama Rose angenifanyia hivi maana nilimwamini sana, nafanya naye kazi nyingi na hiyo fedha alikwenda nayo kwenye mkutano Nairobi (Kenya).
“Kutokana na hali hiyo niliamua kuikimbia nyumba yangu, maana mke wangu najua anahisi mimi simdai Rose labda ni mpenzi wangu, lakini sivyo.”
“Kilichonikimbiza nyumbani ni kelele za kila siku kutoka kwa mke wangu, nina miezi mitatu sijafika, naumia sana na sijui itakuwaje. Kila nikimpigia simu Rose ananizungusha tu, daa!”

ALIMPAJE ROSE FEDHA HIZO?
Daudi alipoulizwa namna alivyomkabidhi pesa hizo Rose, alijibu: “Rose alikuwa na ishu kubwa Kenya hivyo alimtuma ndugu yake aje Mbezi, nikamkabidhi pesa hiyo mikononi bila kuandikishana popote kwani nilimwamini kwa kuwa wote sisi ni watumishi wa Mungu.”

ROSE: SUBIRI DAKIKA MOJA
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimtafuta Rose aeleze ukweli juu ya sakata hilo ambapo alipopigiwa simu na kuelezwa mkasa mzima alimwambia mwandishi wetu asubiri dakika moja.
Hata hivyo, baada ya dakika kumi alipigiwa tena lakini akawa anapokea bila kuongea.

Mwimba Injili ‘grade one Bongo’, Rose Muhando
Baadaye, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno  (SMS) wenye madai yote ili kama alikuwa sehemu mbaya kuongea ajibu kwa njia hiyo lakini hakufanya hivyo.
MWENYE USHAHIDI AJITOKEZE
Kutokana na Rose kuwa na madai mengi ya kuingia mitini na fedha za watu, waandishi wetu walimtafuta Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel ili kutoa ufafanuzi wa nini wamepanga kukifanya juu yake.

“Tumekuwa tukisikia tu, hatujapata ushahidi,  tukisikia amepelekwa polisi au mahakamani tutatoa tamko lakini kwa sasa hatuwezi kwa sababu mwenyewe huwa anasema anazushiwa, mambo ya Rose ni makubwa kwa kweli.”
KUNA TATIZO?
Hivi karibuni Rose alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja alizopewa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimba Injili, John Lissu uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar.

Kama hiyo haitoshi, Jumapili iliyopita, Rose tena alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni mbili za watu alizolipwa ili kushiriki tamasha moja lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Land Mark Hotel, Ubungo, Dar.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MKE: ROSE MUHANDO KANIHARIBIA NDOA
MKE: ROSE MUHANDO KANIHARIBIA NDOA
http://api.ning.com:80/files/Ugvao0mAfe4RwhwmokP0WjcOiH4weYzz*4-51OncxOXLsoUda0gQCYEPTI5NjJYd5IGBMW6VTXFHh1lgE6PZL4vB8ULpPGiS/IMG_7498.JPG?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mke-rose-muhando-kaniharibia-ndoa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mke-rose-muhando-kaniharibia-ndoa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago